Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.\
Immaculate Makilika - MAELEZO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga amesema Tanzania na Vietnam zimeahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali kufutia makubaliano yaliyofanyika wakati wa ziara ya Rais wa Vietnam nchini.
Waziri
Mahiga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi
wa habari wakati wa majumuisho ya ziara ya siku nne ya Rais wa Vietnam
nchini Mheshimiwa Truong Tan Sang.
Akiwa ameongozana na Waziri Habari na Mawasiliano wa Vietnman Nguyen Bal Son ameyataja maeneo ambayo Tanzania na Vietnam zimekubaliana kushirikiana kuwa ni uwekezaji wa kilimo cha mpunga, uvuvi wa samaki wa ziwani na baharini na uanzishwaji wa viwanda vya kusindika mazao ya biashara.
“Tumekubaliana
kushirikiana katika maeneo kadhaa ikiwemo kuimarisha uhusiano wa
kidiplomasia, kuongezeka kwa uwekezaji kutoka Vietnam kwani kwa sasa
biashara inayofanyika kati ya Vietnam na Tanzania ni dola milioni 300
kwa mwaka, tumekubaliana ifikie dola bilioni 900 ifikapo mwaka 2020”
Aidha,
maeneo mengine ya ushirikiano ni pamoja na kufungua mahusiano ya
mawasiliano na elimu, ambapo kutakua na fursa kwa wanafunzi wa
Kitanzania kwenda kusoma nchini Vietnam, na wataalamu wa Vietnam kuja
kufanya kazi pamoja na watanzania na kusema kuwa kampuni ya simu ya
Halotel imefungua mlango kwa Vietnam kuwekeza nchini na kuongeza kuwa
lengo la ushirikiano huu ni kuwa na uhusiano ulio sawa na kila mmoja
anufaike na mahusiano hayo.
Hata hivyo, Mahiga amesema kuwa pamoja na maeneo kadhaa waliyokubaliana jambo la msingi ni namna ambavyo nchi hizo zitatekeleza makubaliano hayo kwa kuwa na mawasiliano ya karibu na kukutana mara kwa mara baina ya watendaji wa Serikali hizo mbili.
Rais
wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang, aliwasili nchini machi 8 mwaka huu,
ambapo alikutana na Rais Mhe. John Magufuli na kufanya mazungumzo Ikulu
na kutia saini mkataba wa kibiashara baina ya Tanzania na Vietnam.
Aidha,
Rais Truong na ujumbe katika ziara yake ya siku nne nchini alikutana na
Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete, alizungumza na jukwaa la
wafanyabiashara na viongozi wao, na pia alitembelea eneo la viwanda (EPZA) Ubungo jijini Dar es salaam.
Vilevile,
alifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Job Ndugai na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.
Dkt. Ali Mohamed Shein ambapo walikubaliana kuwa na mahusiano ya karibu
na visiwa vya Zanzibar kwa ajili ya uwekezaji katika utalii na uvuvi wa
samaki.
Kwa
upande wake, Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Vietnam Mhe. Nguyen Bal
Son amesema nchi yake ina historia nzuri ya ushirikiano na mahusiano ya
kidiplomasia ya muda mrefu yaliyo asisiwa na Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na hivyo wataendeleza uhusiano huo na Tanzania pamoja na
kushirikiana ili kukuza uchumi wa nchi hizo.
0 comments:
Post a Comment