Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania wamefundishwa jinsi ya kutunga
sheria ikiwa ni moja kati ya kazi muhimu za Bunge katika semina za
kamati mbalimblai za Bunge zinazoendelea kufanyika Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yametolewa leo katika semina ya kamati ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Utawala na TAMISEMI zilipokutana
kujadili mambo mbalimbali yahusuyo kamati hizo ikiwa ni njia ya kuwakumbusha wabunge wajibu wao.
Akiwasilisha mada kuhusu kazi za Bunge na kamati zake kwa wabunge,
Mkurugenzi Msaidizi wa Bunge Michael Chikokoto amesema dhumuni la semina
hiyo ni kuwakumbusha wabunge wajibu wao ikiwemo suala la utungaji wa
sheria za nchi.
“ Wabunge kazi yao sio kudhamini miradi tu ya maendeleo katika majimbo
yao bali kuisaidia Serikali katika kuwasilisha mambo muhimu kwa
kuwasilisha miswaada itakayopelekea kuwa sheria ambazo zitasaidia
kuiendesha nchi” Alisema Chikokoto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama Mhe. Balozi Adadi Rajabu Mbunge
wa Muheza amesema semina hizi ni muhimu kwa wabunge kwani zinawawezesha
kuwapa uelewa wa kutosha katika masuala ya uuandaaji wa miswaada
kuanzia mwanzo mpaka inapokuwa sheria.
” Semina hizi zinatupa mwanga hasa kwa wabunge wageni katika Bunge kujua
ni kwa namna gani wanaweza kuandaa na kuwasilisha miswaada ikiwa ni
pamoja na miswaada binafsi ama miswaada kupitia kamati mbalimbali za
Bunge” Alisema Balozi Rajabu.
Aidha naye Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na TAMISEMI Mhe. Jasson
Rwekiza Mbunge Bukoba Vijijini amesema mbali na kuwawezesha wabunge
kuelewa jinsi ya kutayarisha miswaada mpaka kuwa Sheria pia kamati hizi
zina kazi ya kuangalia, kufatilia na kuhoji matumizi ya fedha za bajeti
ya Serikali.
Kamati mbalimbali za Bunge zinakutana Jijini Dare s salaam ili kujadilia
mambo mbalimbali yahusiyo kamati hizo kabla ya kuanza kwa mkutano wa
tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotarajiwa
kuanza mwezi Aprili.
0 comments:
Post a Comment