Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Kampuni
ya Moovn Tanzania Limited imeboresha huduma za usafiri na kuongeza
usalama wa wateja kwa kuanzisha huduma za usafiri zinazopatikana kwa
njia ya mtandao.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni
hiyo,Bw.Godwin Ndugulile alipokua akiwaelekeza waandishi wa habari jinsi
ya kujiunga na huduma za usafiri kwa njia ya mtandao.
“Huduma
zetu za usafiri zinapatikana kwa njia ya simu na tovuti kupitia program
za aina tatu ambazo ni programu inayomuhusu mteja,(Moovn Passenger),
programu inayomuhusu dereva (Moovn Driver) pamoja na Programu
inayohusiana na mashirika au makampuni ya kibiashara”alisema
Bw.Ndugulile.
Bw.Ndugulile
ameongeza kuwa huduma hizo zinapatikana bure kwa wateja wote pia
kampuni inashirikiana na madereva wa vyombo vya usafiri wa aina zote
zikiwemo taxi, pikipiki, na bajaji ili kutoa huduma nafuu kwa wateja
wao.
Aidha,
Bw. Ndugulile amezitaja baadhi ya faida zinazopatikana kwa kutumia
huduma hii kuwa ni; usafiri wa uhakika kwa kuwa madereva wote wana
leseni na wamesajiliwa, usalama, bei nafuu kulingana na mahitaji na
uwezo wa mteja, pamoja na kuongeza ajira na kipato kwa madereva.
Kampuni
ya Moovn Tanzania Limited imeanza kufanya kazi rasmi Machi 16 Mwaka
huu, Ofisi zake zinapatikana maeneo ya Osterbay Jijini Dar es Salaam pia
Kampuni ina mpango wa kufungua matawi mengine nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment