Na Beatrice Lyimo - MAELEZO
21/04/2016 Dar es Salaam
Wadau
mbalimbali kutoka vyama vya Siasa vilivyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu
uliofanyika Octoba 25, 2015 wameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
kwa kuendesha zoezi hilo kwa Uwazi, Haki, Amani na kwa kuzingatia
Sheria na Kanuni.
Hayo
yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Chama cha NRA Bw. Hassan Kasabya
alipokuwa akitoa pongezi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kutoa vyeti
vya shukrani kwa washiriki hao katika huo kwa vyama vya siasa na wadau
wengine.
Bw.
Kasabya amesema kuwa Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliona umuhimu wa vyama
hivyo kama wadau wa uchaguzi na chaguzi zote hapa nchini na kuamua kutoa
kutoa vyeti vya shukrani kwa kufanikisha uchaguzi huo.
“Vyeti
hivi ni kielelezo tosha cha umakini wa Tume yetu na jinsi gani wamejali
na kuthamini ushiriki wa vyama vyetu, kwani pasipo vyama vyetu hivi
uchaguzi mkuu hauwezi kufanyika” ameongeza Katibu Mkuu huyo.
Aidha,
kwa upande wake Katibu Mkuu kutoka Chama cha AFP Rashid Rai ametoa wito
kwa Serikali kuzidi kuiwezesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi hususan
uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kuzidi kutoa elimu ya
uraia kwa wapiga kura.
Mbali
na hayo, Wadau hao wameipongeza Tume hiyo kwa mabadiliko makubwa ya
kiutendaji yaliyofanyika katika uchaguzi mkuu uliopita kulinganisha
uchaguzi wa mwaka 2010, 2005, 2000 na 1995.
Wadau
walioshiriki kuipongeza NEC kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana ni
pamoja na Chama cha National Alliance and Reconstruction (NRA), Chama
cha Alliance for Tanzania Farmers (AFP), Chama cha United Peoples
Democratic Party (UPDP), Chama cha UMD, Chama cha Demokrasia Makini
(MAKINI) na Chama cha Haki na Ustawi (CHAUSTA).
0 comments:
Post a Comment