Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake
wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na
viongozi wa Foundation For Women of Africa na wafadhili wa mradi huo, mara
baada ya uzinduzi wa mradi huo Madrid, Spain hivi karibuni.
Mama Maria Tereza (katikati) - Rais wa taasisi ya Foundation
for Women of Africa akiwa na waandishi wa habari wanaotekelza mradi wa Green
Voices wakati wa hafla ya kuwakaribisha kinamama nchini Spain. Kutoka kushoto ni Secelela Balisidya, Tukuswiga Mwaisumbe, Farida Hamis,
Siddy Mgumia na aliyechuchumaa Judica Losai.
Akinamama wanaoshiriki katika
mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi –
Green Vocies katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo kikuu cha Universitad
Automous De Madrid, mara baada ya kutembelea mazingira ya chuo hicho Madrid,
Spain hivi karibuni.
Ziara ya mafunzo kujifunza
jinsi ya kutengeneza mbolea ya mboji.
Ziara ya mafunzo kujifunza
majiko yanayotumia nishati ya jua.
Ziara ya mafunzo katika chumba
cha habari cha gazeti la El Pais.
Akimama na wawezeshaji wa
mafunzo katika picha ya pamoja darasani.
WANAWAKE wapatao 15 hivi karibuni walihudhuria mafunzo ya kuongeza ujuzi
wa jinsi ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi nchini Spain. Mafunzo na mradi
huo vinafadhiliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika,
ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu waSpain Mama María Teresa Fernández de laVega.
Taasisi hiyo itafanya kazi na wanawake hao 15 wa kitanzania kupitia miradi
inayosaidia nchi kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Wanawake hao ambao kati
yao watano ni waandishi wa habari kila mmoja atatekeleza mradi mmoja, huku
waandishi wa habari wakisaidia kupaza sauti za akinamama hao kupitia vyombo
mbalimbali vya habari nchini.
Mradi huu unaojulikana kama GREEN VOICES una lengo la kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii
nzima ya kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika
kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Mradi huo unaoratibiwa hapa nchini na Mtandao wa wanahabari wa Mazingira
(EMNet) kwa niaba ya Foundation for Women of Africa unatekelezwa katika mikoa
sita ya Kigoma, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani ukihusisha
miradi ya kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.
Mratibu wa EMNet Secelela Balisidya amesema akinamama hao wanatekeleza
miradi ambayo inachangia moja kwa moja aidha kupambana au kupunguza athari za
mabadiliko ya tabianchi. Amesema miradi hiyo ni mradi wa kilimo cha miti ya
matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza,
Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani na ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia
nishati ya jua mkoani Morogoro. Miradi mingine ni usindikaji wa vyakula
mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga na kilimo
cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa
utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro.
Mradi huo unaotarajiwa kutelekezwa kwa mwaka mmoja unatoa fursa kwa kinamama
kutoa ujuzo wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi na sauti zao kusikika.
Hiyo ni kwa sabuabu kinamama wana uhusiano mkubwa na mazingira kutokana na kazi
wanazozifanya kila siku za kilimo na utunzaji wa familia kuhusiana moja kwa
moja na mazingira hivyo kuyaelewa zaidi mazingira na jinsi ya kupambana na
mabadiliko ya tabianchi.
Wakiwa Madrid nchini Spain walikopata mafunzo wa wiki mbili katika chuo
kikuu cha Autonomus Universitad De Madrid, akinamama hao na waandishi wa habari
walijifunza kwa nadharia na vitendo jinsi nchi ya Spain inavyokabiliana na
mabadiliko ya tabianchi na kuona njia ambazo na huku nchini zinaweza kutumika
kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Mafunzo kwa vitendo pia yalihusisha ziara
za mafunzo kujifunza kilimo hai, na jinsi nishati jua inavyoweza kusaidia
kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Waandishi wa habari pia walipata nafasi ya kutembelea chumba cha habari
cha gazeti la Serikali ya Sapin la El
Pais an kujifunza zaidi jinsi waandishi wa huko wanavyoandika habari
zihusianazo na mabadiliko ya tabianchi.
Tovuti: Green Voices
0 comments:
Post a Comment