Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es Salaam.
KAMPUNI ya Dream Success
Enterprises kwa kushirikiana na kampuni ya Bid Production wameanzisha
mfumo mpya wa kiuchumi ujulikanao kama “Life Formula Family (LFF)” kwa ajili ya kubuni masoko na mtaji katika tasnia ya Sanaa nchini.
Mfumo huo unatarajia kuzalisha
wawekezaji Wazawa na Wafanyabiashara wakubwa na hivyo kuipaisha sanaa ya
Tanzania katika ngazi za kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Bid Production,
Bw. Fadhili alisema kuwa kampuni hiyo ina lengo la kuhamasisha wahitimu
wa vyuo vikuu nchini kuanzisha makampuni na kujiajiri na hivyo
kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana.
Matekela alisema kuwa mfumo huo wa Life Formula Family unatarajia kuanza na Watu Milioni 5, ambapo mwanachama atakejiunga atapatiwa namba maalum ya utambulisho..
“Filamu zitakazoingizwa katika
mfumo huu zinatarajiwa kuuzwa Tsh. 3,000 kwa wakazi wa jijini dare s
salaam na kwa upande wa wakazi wa mikoani itategemea na gharama za
usafirishaji” alisema Mateleka.
Aliongeza kuwa kampuni yake pia
inatarajia kuendesha kongamano maalum lijulikanalo kama la “Sitaki
kuajiriwa” ambalo litawahusisha wahitimu wa vyuo vikuu nchini, ambapo
watajadiliana kwa pamoja tatizo la ajira kwa vijana na hatua za
kukabiliana na tatizo hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Dream Success Enterprises, Charles Makoba alisema taasisi
imeunga mkono kwa vitendo Hatua za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mkakati wa kutumbua majipu, hivyo taasisi yake imekusudia
kutumbua jipu la ukosefu wa ajira kwa vijana.
“Tumeamua kuanzisha kampeni ya
“Sitaki Kuajiriwa” kwa kuhimiza wahitimu na wanavyuo kuanzisha makampuni
yao, na tayari kampuni ya kwanza ya Bid Production imeshajiliwa na
tumeungana katika kuendesha kampeni ya Sitaki kuajiliwa” alisema Makoba.
0 comments:
Post a Comment