Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji kumwandikia Kamishna wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania(TRA) kuomba taarifa za mapato halisi za benki zilizopo
Dar es Salaam ili kujiridhisha na kiwango kinachotolewa na benki hizo
wakati wa kulipa ushuru wa huduma za Jiji(City Service Levy).
Akizungumza Jijini
Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita amesema kuwa kutokana na kutoridhishwa
na taarifa ya mapato iliyotolewa katika baraza la madiwani la
Halmashauri ya Jiji hilo,lililofanyika Mei 02 mwaka huu ikionesha mapato ni madogo kulingana na wingi wa vyanzo vya mapato vilivyopo.
“ Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea kuhusu vyanzo vya mapato vya
Halmashauri ya Jiji haviendani na vyanzo vilivyopo hasa ushuru utokanao
na huduma za Jiji zinazotolewa kwa mabenki mbalimbali yaliyopo ndani ya
Halmashauri” Alisema Mwita.
Mstahiki Mwita ameongeza kuwa ingawa Halmashauri inapata taarifa za
benki kutoka Benki Kuu (BOT) lakini kumekuwa na mkanganyiko wa uwiano wa
makusanyo ya mapato na idadi ya benki zilizopo zinazopatiwa huduma za
Jiji hivyo ameagiza kupata ufafanuzi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA) ili kujiridhisha.
Aidha Mstahiki Meya amempa Mkurugenzi wa jiji hilo, wiki moja kuwasilisha taarifa yenye orodha ya idadi ya benki zilizopo katika Jiji la Dar es Salaam na zinazotakiwa kulipa ushuru.
Kwa mujibu wa sheria za huduma ya Jiji watumiaji wote wa huduma hizo wanatakiwa kulipia ushuru wa huduma hizo kwa
wakati na kuwataka kulipa ushuru uliopo kwani sio majadiliano bali ni
sheria na wanatakiwa wazifate kwa maendeleo yao na ya Jiji.
0 comments:
Post a Comment