Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu
(SUMATRA) Bw. David Mziray akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau wa usafiri wakiwamo SUMATRA,
UDA, DART na Jeshi la Polisi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA)
Bw. Giliard Ngewe akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani)
kuhusu nauli zitakazotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka
unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 10, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Udhibiti Uchumi kutoka SUMATRA Bw. Nahson Sigala.
Mkurugenzi
wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi
Kavu (SUMATRA) Bw. Nahson Sigala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu
viwango vipya vya nauli baada ya SUMATRA kufanya tathmini ya viwango vya
nauli iliyopendekezwa awali na Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT na
kubaini kuwa gharama zilizopendekezwa ni kubwa mno. Kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw.
Giliard Ngewe.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA)
Bw. Giliard Ngewe (Kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu DART Bw. Ronald
Lwakatare wakimkabidhi leseni ya usafirishaji Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Katikati).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa
(Kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa
Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe baada ya kupokea leseni
ya usafirishaji kutoka SUMATRA.
PICHA NA FATMA SALUM-MAELEZO
0 comments:
Post a Comment