Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » IOM YAWAFUNDA VIJANA WALIO MASHULENI NA WALE WA MTAANI

IOM YAWAFUNDA VIJANA WALIO MASHULENI NA WALE WA MTAANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Shirika lisilo la kiserikali, International  Organization for Migration,(IOM) limeendesha mafunzo ya siku moja kwa zaidi ya vijana 150 waliyopo katika Vyuo Vikuu,Sekondari  na wale wa mitaani lengo ni kuwapa elimu na kufahamu  faida za kiusalama za Uhamaji. 

Akifungua mafunzo hayo katika, Hotel Coral Beach iliyopo Masaki jijini ,Afisa Miradi wa shirika hilo Charles Mkude, amesema kuwa lengo la kuwakutanisha vijana hao ili kuwajengea uwezo wa kutambua mambo mbalimbali yatokana na Uhamaji na kujua faida na hasara zake.

“Uhamaji sio tatizo la nchi pekee, bali tatizo la ulimwengu mzima ni wajibu wetu kufanya hivi kila mara maana kundi kubwa la vijana wakielimishwa basi kama taifa tunaweza kupiga hatua moja mbele lengo kubwa ni kueleza maswala jinsi gani jamii inaweza kufaidika na  uhamaji kwa fuata taratibu  sahihi za kiusalama,unajua wengi utumia mwaya huu uhamaji  kwa kufanya biashara haramu  za utumwa katika mataifa mbalimbali iwapo kila kijana ataelewa kwa kina kuhusu mafunzo haya basi atapeleka ujumbe katika jamiii na kuwa barozi mzuri ili mwisho wa siku yatumike maamuzi ya kibusara kama taifa”alisema Mkude.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa