Na Daudi
Manongi-MAELEZO
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan leo hii amezindua jukwaa
la kuwezesha wanawake na akaunti maalum ya mikopo ya MALAIKA inayolenga
kuwawezesha wanawake wa hali ya chini kiuchumi kupitia Benki ya wanawake katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akiongea katika uzinduzi
huo Mheshimiwa Samia Suluhu amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa jukwaa hilo ni
kuwapa uwezo wanawake waweze kutoka katika sekta isiyo rasmi na kuingia katika
sekta rasmi na hivyo kuwainua kiuchumi kwani mchango wa mwanamke mpaka sasa
bado haujaongezeka thamani.
Aidha Bi Samia ameagiza
kuwa kuanzia sasa asilimia 35% ya tenda za serikali za mitaa ziende kwa
wanawake na vijana ili kuwawezesha kiuchumi na kuwataka wanawake kubadilika kifikra
na hata wanapopata mikopo hii wawe na nidhamu katika matumizi yake.
Hata hivyo Mhe.
Suluhu ametoa rai kwa mabenki kufikisha huduma zao vijijini ili huduma ya mikopo iwafikie wanawake wachangie
uchumi wa dunia na sio tu kwa familia huku akiwahimiza wanawake
kupendana,kushirikiana na kusaidiana.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Dkt.Hamisi Kigwangala
amesema kuwa serikali imeendelea kusaidia wanawake katika Nyanja mbalimbali
ikiwemo kuweka usawa wa jinsia kwa wanawake kiuchumi ,kutoa vikwazo katika
masoko na kuondoa mila kandamizi.
Aidha Dkt Kigwangala
ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa
wanawake kwa kufanya mafunzo ya ujasiliamali na kuweka sera nzuri ambayo yote
haya yameainishwa katika ilani ya chama cha mapinduzi ya 2015-2020 uku akieleza
mafanikio makubwa ya benki ya wanawake ambayo mpaka sasa imetoa mikopo yenye
thamani ya bilioni 86.
Uzinduzi wa Jukwaa
hilo na akaunti ya MALAIKA ya mikopo uliendana na mada mbalimbali kutoka kwa
wadau mbalimbali kama Crdb,Benki ya wanawake,Nssf ,Wizara ya Viwanda na
Biashara na Tcra.
0 comments:
Post a Comment