Mganga
Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi, akizungumza na waandishi
wa habari nje ya Ukumbi unaofanyika Mkutano wa Pili wa Neuroradiolojia
jijini Dar es Salaam, unaojadili Jukumu la Neuroradiolojia katika
kukapambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.
Msajili
Mstaafu wa Baraza la Wataalamu wa Radiolojia (MRIPC) Euniace Bandio,
akizungumza kuwakaribisha Wataalamu na Washiriki wa Mkutano wa Pili wa
Neuroradiolojia unaofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa siku
mbili unajadili Jukumu la Neuroradiolojia katika kukapambana na Magonjwa
Yasiyoambukiza.
Katibu
wa Jukwaa la Neuro-rad Dkt. Mboka Jacob akizungumza na washiriki wa
mkutano wa Pili wa Neuroradiolojia unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watalaamu wa Radiolojia na washiriiki wa mkutano huo wakimsikiliza mgeni rasmi.
Hussein Makame-MAELEZO
SERIKALI imesema haitamvumilia
mtumishi yeyote wa sekta ya afya atakayefanya kazi zake bila kuzingatia
weledi na maadili ya taaluma za sekta hiyo.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa
Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi, wakati akifungua Mkutano wa Pili
wa Neuroradiolojia ulioanza jijini Dar es Salaam leo, kujadli Jukumu la
Neuroradiolojia katika kukapambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.
Prof. Kambi alisema ametoa
msimamo huo kutokana na ukweli kwamba wataalamu wa sekta hiyo
wanashughulikia afya ya binadamu kwa hiyo ni lazima wafanye kazi zao kwa
kuzingatia weledi na maadili.
“Mtu yeyote ambaye ni mtumishi
katika sekta ya afya ni lazima afanye kazi zake kwa kuzingatia weledi na
maadili ya taaluma, hivyo ndivyo taaluma zetu kwenye sekta ya afya
zinavyotaka” alisema Prof. Kambi na kuongeza kuwa:
“Kwa hiyo mtu ambaye hatafuata
weledi na maadili sisi kama Serikali hatutaweza kumvumilia kwa sababu
tunashughulikia afya ya binadamu kwa hiyo ni lazima kazi hizi tuzifanye
kwa kuzingatia weledi na maadili”
Kuhusu mkutano huo, Mganga Mkuu
huyo wa Serikali, aliwaomba washiriki wa mkutano huo kuangalia na
kujadili changamoto mbalimbali za taaluma ya Neuroradiolojia ili
waisaidie Serikali kupata mawazo na ushauri wa jinsi ya kuzitafutia
ufumbuzi changamoto hizo.
Akizungumzia vifaa muhimu katika
hospitali za Kanda nchini, Prof. Kambi alisema Serikali inafanya
jitihada za kuhakikisha hospitali zote za Kanda angalau zihakikishe
zinapata vifaa vya Ultrasound, CT Scan na MRI ambazo ni muhimu katika
kutoa huduma za afya.
Aliongeza kuwa hali si mbaya
katika vituo vya afya kuhusu masuala ya vipimo kwa sababu hospitali
nyingi za Serikali zina vipimo vikubwa muhimu kwa utoaji wa huduma ya
afya kwenye hospitali hizo.
“Kwa mfano kwenye Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili tuna Ultrasound, tuna CT Scan, tuna MRI.Ukienda
hospitali ya Bugando baadhi ya vipimo vipo vingine havipo, ukienda
kwenye Hospitali ya Kanda ya Mbeya nako kuna baadhi vipo na vingine
havipo” alisema na kufafanua kuwa:
“Lakini sisi kama Serikali
tunafanya jitihada za kuhakikisha hospitali zote za Kanda angalau
zihakikishe zinapata vifaa vyote hivi ambavyo ni muhimu katika kutoa
huduma za afya”.
Kwa upande wake Mkufunzi
Muandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili na Mwenyekiti wa Baraza la
Walaamu wa Radiolojia Nchini (MRIPC) Dkt. Ramadhani Kazema alisema
jukumu la baraza hilo ni kuangalia kama wataalum wa Radiolojia wanakidhi
mahitaji katika mafunzo na wanafanya kazi zao kwa weledi.
“Changamoto zinazoikabili tasnia
hii katika nchi hasa za Afrika ni uhaba wa fedha na kuna jitihada
zimefanywa ili kuboresha upatikanaji wa fedha kama unavyojua bajeti za
hospitali ni kidogo ziko finyu kwa hiyo inakua na athari kwenye utendaji
wetu wa kazi” alisema Dkt. Kazema.
Alifafanua kuwa pamoja na
wataalamu wa Radiolojia kuwa si wa kutosha lakini wanaridhisha na
vitendea kazi vipo vinaridhisha ,ingawa changamoto ni jinsi ya kuvifanya
vitendea kazi hivyo viendelee kufanya kazi kwa muda wote.
Mkutano huo wa siku mbili wa
Wataalamu wa Nuerolojia unajadili Mada kuu inayosema “Jukumu la
Neuroradiolojia katika kukabialiana na Magonjwa Yasiyoambukiza na
kushirikisha wataalamu kutoka Kenya, Marekani, Uganda, Korea Kusini,
Uingereza na Tanzania.
Hata hivyo, mkutano huo pia
unatarajia kushirikisha wataalamu hao kubadilishana uzoefu na utaalaamu
katika masuala ya Neuroradiolojia na kujadili masuala ya ugonjwa ya
kansa ya matiti.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Unyayo wangu ni kipindi kipya kabisa kinachokujia kupita Tone Tv,
ambacho kinaletwa kwenu na Mtangazaji wetu Eddie Nyota , kinacholenga
shabaha ya watu waliothubutu kufanya jambo fulani katika jamii na
wanauelewa na jamii husika. Utajifunza mengina kuburudika pia kupitia
kipindi hiki Kinacholenga rika zote.

0 comments:
Post a Comment