Kampuni
ya Shear Illusions imehadhimsha mwaka mmoja tangu uzinduzi wa Kipodozi
Pendwa cha LuvTouch Manjano. Kipodozi cha LuvTouch kilizinduliwa mnamo
tarehe 31 May mwaka 2015 jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi aliyekuwa
mke wa Waziri Mkuu wa zamani Mh. Mama Tunu Pinda katika ukumbi wa
Diamond Jubilee. Katika maadhimisho hayo Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear
Illusions mama Shekha Nasser amewashukuru wanawake na Watanzania kwa
ujumla kwa kufanikisha kutambulika kwa bidhaa za LuvTouch Manjano.
LuvTouch ni Brand ya Kipodozi cha kwanza nchini inayomilikiwa na
mwanamke mzalendo wa Kitanzania. Kupitia bidhaa hiyo pia imeanzisha
Taasisi ijulikanayo kama 'Manjano Foundation' yenye lengo kuu ya
kuwasaidia wanawake kiuchumi. Katika mwaka mmoja tangu uzinduzi wa
bidhaa za LuvTouch Manjano, Taasisi hiyo imefanikiwa kuwaelimisha zaidi
ya wanawake 195 katika mikoa mitano nchini. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam,
Mwanza, Zanzibar, Arusha na Dodoma.

Pia
katika kipindi cha mwaka mmoja wameweza kuwakopesha wanawake mitaji ya
vipodozi vya LuvTouch Manjano yenye thamani ya shilingi milioni 45
(TSh.45,000,000). Akieleza zaidi mama Shekha Nasser amesema ataendelea
kuwashika mkono wanawake wenzake kadiri ya uwezo wake unavyoruhusu kwa
lengo la kumkomboa mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la
ukosefu wa Ajira.Maadhimisho
hayo yalihudhuriwa na wanawake walio washiriki wa mradi wa Manjano
Dream-Makers na wadau (Mentors), washauri na watu waliojitolea
kuwasaidia washiriki hao.

Wanawake
na washauri waliohudhuria hafla hiyo walimpongeza mama Shekha Nasser
kwa moyo wake wa kujitolea na kuwabeba wanawake vijana. Mmoja wa
wazungumzaji na mdau wa mradi, mwanasaikolojia maarufu aunt Sadaka Gandi
alisema, ameishi na wanawake wengi nchini lakini hajawahi kuona
Mwanamke mwenye moyo wa kujitolea kama wa Shekha. Amewaasa wanawake
walionufaika na mradi huo kufanya kazi kwa bidii kupitia Mradi huo kwa
kuwa wao wanabahati sana kunufaika kwa kuwa wapo wanawake wengi nchini
wasiokua na kazi na wangetamani kunufaika lakini wamekosa nafasi hiyo


0 comments:
Post a Comment