Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Frank
Mvungi-Maelezo
Serikali
kutumia zaidi ya bilioni 4 kuwawezesha wajasiriamali wadogo katika Manispaa ya
Kinondoni katika Kipindi cha mwaka 2016/2017 ili kuchochea kasi ya ukuachi wa
uchumi.
Kauli hiyo
imetolewa Leo Jijini Dar es salaam na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni
Bw. Sebvastian Mhowera wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Akifafanua
Mhowera amesema fedha hizo zitatolewa kupitia Mfuko wa wanawake na Vijana
unaolenga kuwawezesha kishiriki katika shughuli za uzalishaji hali itakayachangia
kukuza uchumi.
Kwa Sasa
manispaa ya Kinondoni inajumla ya Vikundi 546 vya wanawake na vijana vyenye
jumla ya wajasiriamali 2729 ikilinganishwa na vikundi 40 na wanufaika 200
waliokuwepo mwaka 2013.
Wajasiriamali
wanaonufaika na fedha za mfuko huo ni wale wanajishughuisha na shughuli za
Kiuchumi ikiwemo kilimo,Biasharandogondogo,Ushonaji,Ufugaji,Uvuvi,Mafundi
seremala,wasusi.
Pia Mhowera
alitoa wito kwa wajasiriamali wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza kuchangamkia fursa zinazotokana na mfuko wa
wanawake na vijana.
Kuanzishwa
kwa mfuko huu katika manispaa ya Kinondoni ni utekelezaji wa agizo la Serikali
Kuu lililoagiza Halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa
ajili ya mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana.
Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni inaandaa maonesho kwa ajili ya wajasiriamali wadowadogo wanaonufaika na Mikopo ya Mfuko wa
wanawake na vijana inayotolewa na Manispaa hiyo ambapo maonesho hayo
yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment