Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemteua Bw.
Eliud Nyauhenga kuwa Kaimu Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB).
Kwa
mujibu wa taarifa ya Waziri huyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo
Jijini Dar es Salaam inaeleza kuwa, uteuzi huo umefanyika baada ya
Meneja wa Bodi hiyo Bw. Joseph Haule kumaliza mkataba wake.
“Kwa
mamlaka niliyonayo chini ya Sheria ya Bodi ya Mfuko wa Barabara Sura
220 ya mwaka 2006, nimemteua Bw. Eliud Nyauhenga kuwa Kaimu Meneja wa
Bodi ya Mfuko wa Barabara tangu Julai 27 mwaka huu”, alisema Mbarawa.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa, kabla ya uteuzi huo Bw. Eliud Nyauhenga alikuwa Meneja Msaidizi wa Bodi hiyo.
Aidha,
katika taarifa hiyo, Waziri huyo amempongeza Bw. Joseph Haule kwa
kuuongoza Mfuko huo kwa weledi, uadilifu na mafanikio makubwa tangu
ulivyoanzishwa mwaka 2000.
Bodi
ya Mfuko wa Barabara ilianzishwa kwa Sheria Na. 11 ya mwaka 1998 chini
ya Sheria ya Ushuru wa Barabara Na.2 ikiwa na jukumu la kusimamia
makusanyo, matumizi na ufuatiliaji wa Bodi hiyo,
0 comments:
Post a Comment