Na Beatrice Lyimo
MAELEZO
Dar es Salaam
WASANII
wa Filamu nchini wanatarajia kunufaika na kazi zao kufutia makubiliano
ya Kampuni ya Star Media Tanzania Ltd (Startimes), pamoja na Steps
Entertainment za kutumia kazi zao kwenye vituo vya televisheni nchini.
Akizungumza waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Sibuka Media, Dkt. George Nangale alisema
kazi hiyo itafanywa kwa ushirikiano na taasisi hizo ili kuweza
kuwasaidia wasanii kunufaika na kazi zao kupitia luninga badala ya
kuwasubiri wateja wao kuzinunua katika santuri (DvD).
“Tumefikia
uamuzi huu baada ya kuona ombwe lililopo sasa katika kuzifikisha filamu
zetu kwa walio wengi pamoja na kwamba Watanzania wana mwamko mkubwa wa
kuzitazama filamu hizi zenye mafunzo ya maisha na burudani” alisisitiza
Mkurugenzi huyo.
Kwa
upande wake Msanii wa Bongo Movie, Mwanaheri Hamad alisema uonyeshaji
wa kazi zao katika vituo vya televisheni utawanufaisha wasanii chipukizi
ambao kazi zao bado hazijaonekana.
Amesema
kuwa kutokana na mkataba huo wa kurusha filamu hzo umerahisisha soko za
kazi hizo katika mfumo DvD ambapo ulikuwa unatumiwa hapo awali.
Filamu
hizo zitaonyeshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes chaneli 111
ikijulikana kama Sibuka Maisha Steps chaneli kila siku na itaanza
kuonyeshwa Ijumaa hii tarehe 29 Julai, 2016.
0 comments:
Post a Comment