Na Godfriend Mbuya
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ametangaza rasmi , kusitisha maandamano na
mikutano ya siasa iliyokuwa ifanyike nchi nzima kuanzia kesho Septemba Mosi ili
, kupisha nafasi ya viongozi wa dini kukutana na Rais Dkt. John Magufuli
kutafuta suluhu ya kisiasa.
Akizungumza na
waandishi wa habari Jijini Dar es salaam . Mbowe amesema CHADEMA imefikia
uamuzi huo muhimu baada ya vikao na wito kutoka kwa viongozi wa dini wa
madhehebu mbalimbali pamoja na asasi za kiraia.
“Viongozi wa dini na
asasi za kiraia wametuomba, tusitishe maandamano hayo ili wapate nafasi ya wiki
tatu mwezi huu kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Magufuli ili kutafuta suluhu ya kisiasa na kama ikishindikana Octoba Mosi
maandamano hayo yataratibiwa upya” Amesema Mbowe
Aidha Mbowe amewataka
wanachadema na wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu wakati wakisubiri viongozi
wa dini kufanya mazungumzo hayo ili haki yao ya kikatiba iweze kupatikana.
0 comments:
Post a Comment