Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Halmashauri zimeanza kutia moyo- Simbachawene

Halmashauri zimeanza kutia moyo- Simbachawene


Na Godfriend Mbuya
Waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI George Simbachawene amesema halmashauri na mikoa nchini imepiga hatua kubwa katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo ikilinganishawa na miaka ya nyuma.
Akizungumza na kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio , Waziri Simbachawene amesema kwa sasa hali imeanza kuridhisha katika nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na usimamiaji wa miradi ya maendeleo, jambo ambalo linatia moyo katika utendaji wa serikali.

“Hali inaendelea vizuri na kwa kweli kama tukiendelea hivi, kusimamia miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato ya ndani kama tulivyoanza Januari hadi sasa tutapiga hatua kubwa sana katika halimashauri zetu”
Kila fedha ambayo imepelekwa unaiona inapelekwa kwenye maendeleo inatumika kama ilivyokusudiwa na tabia ya kusimamiana imeonyesha kwamba ndani ya muda mfupi wananchi wataanza kufurahia miradi mbalimbali inayotekelezwa sehemu mbalimbali.
Aidha Waziri amesisitiza kwamba mabadiliko ya kizalendo yana dalili ya kufungua Tanzania mpya yenye watu waadilifu na taifa lenye kufuata sheria na utaratibu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa