Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya Zola, akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo, jijini Arusha.
Shughuli za uzinduzi wa duka hilo, jipya la vifaa vya umeme wa jua la Kampuni ya Zola, zikiendelea jijini Arusha.
Wafanyakazi wa Kampuni ya vifaa vya umeme wa jua ya Zola wakishangilia mara baada ya kukatwa utepe wa kulizindua rasmi duka hilo, jipya jijini Arusha.
Wananchi wakiwa katika uzinduzi wa duka hilo, jipya la vifaa vya umeme wa jua la Zola jijini Arusha.
Na Mwandishi wetu,
Arusha, Tanzania (July 28, 2016)
KAMPUNI ya Off Grid Electric, inayomiliki kampuni ya
umeme wa jua ya M-POWER ya Tanzania, imetangaza rasmi leo kubadilisha jina la
biashara (brand name) na ufunguzi wa duka lake la mauzo ya bidha zake kwa
rejareja hapa nchini.
Ufunguzi huo utawasaidia
Watanzania kupata umeme wa jua wenye uhakika kwa bei nafuu kwa matumizi ya
majumbani na katika biashara zao.
Wakati ikiendelea na
kujipanua, Off Grid sasa inabadilisha jina la biashara kutoka M-POWER na kwamba
kwa sasa itajiuza kwa jina la Zola.
Jina
hili la biashara linabeba dhana nzima ya kwamba kampuni hii ina mizizi yake
hapa Afrika Mashariki. Neno Zola limetoholewa kutoka katika neno la Kiswahili
la Solar (Sola) na hivyo litatumika kama jina la biashara la kampuni ya
Off-Grid katika mataifa ya Tanzania na Rwanda wakati kampuni ikijidhatiti
kujipanua zaidi barani Afrika.
Hata
hivyo, kampuni itaendelea kujulikana kwa jina la Off Grid Electric.
“Kutokana na azma yetu ya
kukua zaidi na kufika katika nchi nyingi zaidi hapa barani Afrika, tunahitaji
jina la biashara litakalofanya kazi ndani na nje ya jiografia ya Afrika ili
kuonyesha mtazamo wetu wa mabadiliko katika utendaji,” alisema mwanzilishi
mwenza wa Off-Grid Electric, Bwana Erica Mackey na kuongeza: “Tunaijenga Zola ili
iwe kampuni ya umeme wa nguvu ya Sola kwa Afrika nzima”.
Jina
ya biashara la Zola litazinduliwa rasmi leo (July 28, 2016) kwa ufunguzi rasmi
wa maduka ya mauzo ya bidhaa za Zola Tanzania na Rwanda.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, mkuu wa ubia wa Zola, Bwana Godfrey Kakembo alisema: “Maduka
ya Zola yatawasaidia wateja kujionea jinsi ambavyo bidhaa zetu zinavyfanya kazi
na pia kuweza kuagiza ili waweze kufungiwa sola majumbani mwao. Kwa njia hiyo,
wateja wataweza kutoa Zawadi ya kudumu kwa ndugu, jamaa na marafiki zao waishio
vijijini”.
Katika
maduka ya Zola, wateja wataweza kulipa papo hapo na pia wataruhusiwa kuingia
makubaliano ya kulipa kidogo kidogo.
Wahudumu
kwa wateja watakuwepo muda wote ili kujibu maswali yote yatakayoulizwa na
wateja kuhusiana na bidhaa za Zola.
Waanzilishi wa kampuni na wajumbe wa bodi nao pia watakuwepo ili kushuhudia ukataji utepe utakaoashiria ufunguzi rasmi wa duka la Zola jijini Arusha.
Mwezi
uliopita, kampuni ya Off Grid Electric ilizindua mpango maalum wa kusaidia
kufikisha umeme wa sola unaofaa kwa matumizi ya wajasiliamali wa vijijini.
Mpango huo ulizinduliwa huko California katika mkutano wa kilele uliohudhuriwa
na Rais wa Marekani Barak Obama.
Mpango
huo unajulikana kwa jina la “Kazi na Zola” na unatoa umeme wa kutosha kwa
wafanyabiashara chipukizi kutoka Tanzania na Rwanda kuweza kufanya biashara zao
bila shida, iwe ni biashara ya kinyozi, kuchaji simu, bar na mgahawa kwa
kutumia umeme wa jua.
Kuhusu Off Grid
Electric
Off Grid Electric (OGE), Kampuni
mama ya Zola ni kampuni kubwa inayotoa huduma ya nishati safi, yenye bei nafuu
na inayobadilisha maisha moja kwa moja majumbani. Kampuni inafanya kazi zake
Tanzania na Rwanda. Kwa maelezo zaidi, tembelea: zola.co.tz. or e-mail xxxx
0 comments:
Post a Comment