Home » » KULA MBOGA MBOGA ZINAZOMWAGILIZIWA CHEMBA ZA MAJI TAKA ZA VYOONI NA MAJUMBANI HAKUNA MADHALA KIAFYA NI KINYAA TU-MTAALAM WA KILIMO

KULA MBOGA MBOGA ZINAZOMWAGILIZIWA CHEMBA ZA MAJI TAKA ZA VYOONI NA MAJUMBANI HAKUNA MADHALA KIAFYA NI KINYAA TU-MTAALAM WA KILIMO

Mtaalam mmoja kutoka Wizara ya Kilimo ameeleza kuwa watu kuogopa kula mboga mboga ambazo zinamwagiliwa na kwa kinyesi cha binadamu kutoka katika chemba mbalimbali za maji taka hazina madhara kwa afya ya mwanadamu isipokuwa watu huona kinyaa na kuhofia kupata maradhi.
Alisema kwamba kinyesi hicho pamoja na uchafu mwengine unaotoka kupitia chemba za vyooni huwa na virutubisho na kuongeza kuwa tatizo ni pale wanaposhuhudia umwagiliaji huo na kuona kwa macho yao , na kupata harufu mbaya inayotoka katika maeneo hayo.

Aliongeza kuwa athari anaweza akapata yule anayehudumia mbogamboga hizo kwa kuwa yeye ndiye anayeshika uchafu huo moja kwa moja pindi anapo mwagilizia na pia anapolima.
Hapa ni Sinza nyuma ya Shekilango na huu ni moja ya mtaro unaopitisha maji taka kutoka katika nyumba zilizopo katika eneo hilo na kutumika kwa ajili ya kumwagilia mboga mboga ambazo mwisho wa siku tunazikuta Gengeni na kutumia majumbani.
 Huu ni Mchicha ambao bado unakuwa kutokana na maji hayo
 Mchicha ukiwa unaendelea vizuri kabisa hii ni kutokana na kupata maji hayo yanayotoka katika chemba hizo
Huu ni Mchicha ambao unakaribia kuchumwa na kupelekwa Gengeni kwa ajili ya matumizi ya Majumbani mwetu
Bustani zikiwa katika maandalizi 
Kijana huyu ni mmoja wa wamiliki wa Bustani hizo zilizopo nyuma ya Kituo cha mabasi cha Shekilango, hapa akiwa anamwagilizia Mchicha wake bila hata ya wasi wasi wowote kwa kutumia maji taka ambayo yanatoka katika chemba za vyoo maji haya yanaonekana yana presha ni kutokana na kwamba wanatumia mota kuyasukuma.

Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa Tanzania


0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa