Na Godfriend Mbuya
Msanii
wa nyimbo za Injili nchini Emmanuel Mbasha amesema katika maisha yake
jambo kubwa ambalo anaona fahari ni kumtumikia Mungu na kwa kufanya
hivyo ameona Mungu akimpigania katika mambo mengi magumu.
Akizungumza
na EATV Mbasha amesema kabla hajaokoka alishafanya kazi mbalimbali za
kisanii na makundi ya muziki wa kidunia kwa kufanya Hip Hop lakini
mafanikio yake na amani ya kweli ameiona baada ya kuanza kufanya kazi za
kuhimiz jamii kuhusu habari ya ukuu wa Mungu kwa njia ya uiambaji.
“Mimi
nilikuwa nina rap na akina marehemu Albert Mangwea na wengine wengi ila
nikafika mahali nikaona bila Mungu mambo mengine ni batili hivyo baada
ya kuokoka nimeona Mungu akinishindia mengi na anazidi kunivusha hatua
kwa hatua, ndiyo maana hata kesi yangu Mungu ndiye aliyenipigania
nikashinda na sasa nipo huru”- Amesema Mbasha.
Aidha
Mbasha amesema katika video mpy ambayo ameiachia hivi karibuni ya
‘Haribu Mipango ya Shetani’ ametunga albamu nzima yenye nyimbo 10 ambazo
zipo kwa mtindo wa audio na albamu nzima itakwenda kwa jina la ‘Haribu
Mipango ya Shetani’ ambapo ujumbe wake ni mahususi kwa jamii katika
kuelimisha na kutia moyo juu ya ukuu wa Mungu.
Pamoja
na hayo Mbasha amesema ni vyema vijana wakatambua katika harakati za
kusaka maisha ni vyema kuthamini na kutambua Mungu ndiye muweza wa yote
hivyo kumtegemea yeye kutafanikisha ndoto zao za kusaka maisha.
0 comments:
Post a Comment