Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji
Majenzi kutoka Afrika uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini
Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akihutubia
kwenye mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika.
Rais
wa Chama Cha wakadiriajiMajenzi Afrika Prof. Robert Pearl akihutubia
mkutano wa Wakadiriaji Majenzi uliofanyika kwenye hotel ya Golden Tulip.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza jambo na Viongozi wa Chama cha Wakadiriaji majengo mara
baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa Wakadiriaji Majenzi kutoka Afrika
uliofanyika kwenye Hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
.............................. .........
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa
kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa
ukadiriaji majengo nchini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 18-Aug-16 wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi kutoka nchini mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa
kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya
kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga,
Tanzania na suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa
wakadiriaji majenzi wakajipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo
mikubwa kwa kuweka gharama nafuu kulingana na hali halisi ya mradi
unaotakiwa kujengwa.
Amesema
serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni
muhimu kwa wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi
zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji
majenzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana
uzoefu kwenye kazi zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi
wanayopata.
Kwa
upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa
barabara, madaraja na bandari na viwanja wa ndege hivyo serikali
inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika utekelezaji wa miradi
hivyo na sio vinginevyo.





0 comments:
Post a Comment