Home » » Serikali ya mkoa wa DSM yapiga marufuku UKUTA

Serikali ya mkoa wa DSM yapiga marufuku UKUTA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi Jijini Dar es salaam kuhakikisha kwamba sheria zinafuatwa na kusiwepo kitu kinaitwa UKUTA ili wananchi waendelee na kazi zao kama kawaida.

Akizungumza na kikosi cha kutuliza ghasia katika kambi ya Ukonga Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa askari wanafahamu sheria wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya jambo hilo au maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshaagiza kinachotakiwa ni utekelezaji.

‘’Msisubiri maelekezo yoyote kutoka juu, asiwepo mtu yeyote atafunga duka kwa sababu ya UKUTA nyie ni matrekta hakuna UKUTA unaweza kusimama mbele yenu, mimi kama Mkuu wa Mkoa  ninaamini hatutakuwa na vurugu kwenye Mkoa wetu na hatuwezi kuruhusu vurugu kwa kuwa tunajua madhara ya vurugu’’ Amesema Makonda.

Aidha kwa upande wake Kamanda wa  Oparesheni Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya amesema  jeshi la polisi lipo vizuri na vijana wameandaliwa vizuri na wameandaliwa kuwa tayari siku nyingi na hakuna mtu yeyote atakayethubutu kufanya UKUTA na watakaofanya hivyo watazimwa kabla hawajafanya chocchote.
Kamada  amewaytaka wananchi wote Jijini Dar es salaam kuto jitokeza kwenye oparesheni UKUTA kwa kuwa maadamano hayo siyo halali na watakaojitokeza watapata matatizo yasiyowahusu.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa