Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Serikali yatenga Mil. 900 kuzalisha dawa katika viwanda vya ndani

Serikali yatenga Mil. 900 kuzalisha dawa katika viwanda vya ndani


Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea mbele ya Viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa  nchini(TFDA) hawapo pichani wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akimkabidhi nyenzo za kazi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt. Ben Moses kushoto wakati wa Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) Bw. Hiiti Sillo wa pili kushoto akifafanua jambo kwa Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kulia wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.


Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa maabara za  Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA )wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam

Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Ushauri TFDA wakati wa Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam.
Habari/Picha Na Ally Daud 
Serikali imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje zipatikane nchini.

Akizungumza hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri wa  Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga hatua katika uchumi wa viwanda.

“Serikali kupitia wizara yangu tumetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa kutumia viwanda”.alisema Mhe. Ummy.

Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa kushirikiana na Serikali wanapaswa kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye ubora kwa matumizi ya binadamu ili kupunguza magonjwa yanayotokana na sumu za kemikali zitokananzo na dawa hizo.

Mhe. Ummy ameongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane na Taasisi ya viwango nchini (TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi viwango na ubora unaopaswa kutumiwa na Watanzania.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili kuwawezesha watanzania kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora kwa matumizi ya binadamu .

Mbali na hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa ikusanye mapato kwa wingi zaidi ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga hatua kiuchumi ili isaidie wananchi katika shughuli za maendeleo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt.Ben Moses amesema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri na watayafanyia kazi kwa haraka na ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA KAZI TU”.

“Tumepokea maagizo ya Mhe. Waziri na nataka kumuhakikishia kwamba tutaendelea na kasi yetu ili kuifikisha nchi yetu kwenye kilele cha maendeleo na Afya bora” alisisitiza Dkt. Moses.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa