Na Godfriend Mbuya
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge
amesema taasisi za umma zitawekewa mita za maji ili kuwezesha kukusanya
mapato yatakayosaidia mamlaka za maji nchini kuweza kujiendesha.
Akizungumza
Mkoani Mtwara Mhandisi Lwenge amesema amefikia uamuzi huo baada ya
kupokea malalamiko kutoka kwa Mamlaka ya Maji safi na maji taka mkoani
Mtwara (MTUWASA) kuhusu deni la maji ambalo wanadai taasisi za serikali ambapo kiasi cha milioni 800 jambo ambalo ni kikwazo katika kuendeleza shughuli za kuwahudumia wananchi.
“Baaada
ya kupata malalamiko haya inabidi sasa taasisi za umma ziwekewe mita
ili kuweza kuchangia huduma ya maji na kwa kufanya hivyo mamlaka
zitaweza kujiendesha katika kupeleka huduma na kutatua baadhi ya
changamoto wanazokumbana nazo”Amesema Lwenge
Aidha baadhi ya wananchi mkoani Mtwara wamelalamikia kuchangia huduma ya maji lakini maji yenyewe hawayapati kama ipasavyo.

0 comments:
Post a Comment