Wafanyakazi wa tigo wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo na waandishi wa habari mapema leo katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar es salaam,
Dar es Salaam, Agosti 9, 2016- Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya
kidijitali Tigo Tanzania na kampuni ya Kupatana.com, moja ya kampuni
zinazoongoza Tanzania katika huduma za
masoko katika mtandao zimeingia katika
ubia wa kibiashara ambapo kila kampuni
itauza bidhaa na huduma za kila
mmoja katika majukwaa yao ya kidijitali.
Katika
hatua za mwanzo za ushirikiano huu, Kampuni ya Tigo Tanzania itachagua maduka
matatu ambayo Kupatana.Com itayatumia kuwawezesha wateja wa Tigo kuuza simu zao
zilizotumika kwa kupitia jukwaa la Kupatana.com.
Akizungumza
wakati wa kusaini makubaliano baina ya
pande hizo mbili jijini Dar es Salaam,
Meneja miradi ya biashara wa Tigo, Anthony Njau alisema, “tukiwa ni
kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali, tumeona kwamba hivi sasa Watanzania
wamehamasika mno katika kufanya biashara kupitia njia ya mtandao.”
Njau
aliongeza kwamba , “Mtandao na wavuti wa Kupatana.com unatoa jukwaa zuri ambalo
linabadilisha namna ambavyo watu wanaishi
kwa kuwezesha kupatikana kwa huduma na
bidhaa katika njia sahihi na rahisi.”
“Lengo la muda mrefu ni kuwapatia wateja wetu
jukwaa ambalo wanaweza kupakua vifaa ambavyo vilishatumika ili kuviboresha
na kwa upande wa Tigo kuuza vifaa vipya,
kuongeza usambazaji na kuwa na mafanikio
katika jaribio hili la msingi, Tigo na
Kupatana.com zitapanua wigo wa huduma hii na kuhakikisha inapatikana kwa
urahisi katika maduka yote 52 ya Tigo
ambayo yamesambaa kote nchini,”
alisema Njau.
Mkurugenzi wa Kupatana.com, Philip Ebbersten,
alisema kwamba kupitia matumizi ya jukwaa hilo, wauzaji (kampuni na watu
binafsi) wataweza kuwafikia maelfu
ya wanunuzi muhimu kila siku bila kujali maeneo yao ya kijiografia.
Alifafanua
kuwa kuorodhesha bidhaa katika jukwaa hilo ni bure
na kuwashauru wateja umuhimu wa
kufuata kanuni na miongozo salama
kwa bidhaa zote zitakazotangazwa Kupatana.com ili waweze kuzitapa kwa usalama na uelewa zaidi.
Mwisho .
|
0 comments:
Post a Comment