Viongozi wa kisiasa watakiwa kuwa wavumilivu.
Habari Maelezo
Na Sheila Simba-MAELEZO
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ametoa wito kwa
viongozi wakisiasa Nchini, kuwa wavumilivu ili kulinda Amani ya Nchi.
Sheikh
Alhad ameyasema hayo leo, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam ambapo
amewataka viongozi hao kutii mamlaka iliyoko kwani mamlaka hiyo imewekwa
na Mungu na hivyo ni vema kutafuta njia nyingine kumaliza matatizo
yanapotokea.
“Ipo
haja ya kuvumiliana kwa ajili ya Taifa letu, kwani yanapotokea
machafuko waathirika wakubwa ni wanawake, watoto na vijana wetu ambao
wanaweza kupata madhara makubwa na hata kupoteza maisha’’alisema Alhad
Akizungumzia
maandamano ya ukuta yaliyopangwa kufanyika Septemba Mosi, amesema kuwa
kauli ya kuzuia maandamano hayo imetolewa na Rais wa Nchi na kuomba
kauli hiyo kuchuliwa kwa uzito wa kipekee, kwani busara ni kusikiliza
mamlaka imesema nini na kutii kauli hiyo ya Rais.
“Nawashauri Watanzania
wenzangu, viongozi wangu wa kisiasa jambo hilo si vyema tukashiriki
kwani kutotii mamlaka ni dhambi ndivyo vitabu vya dini vinanavyosema,’’
alifafanua Sheikh Alhad
Ameongeza
kuwa suala la kulinda amani ni la watanzania wenyewe kwa kusaidiana na
Jeshi la Polisi ili kuhakikisha amani inaendelea kuwepo, kwani ni rahisi
kupoteza amani tuliyonayo lakini ni vigumu kurudisha amani.
Amesema
kuwa vijana wasikubali kutumika kwa maslahi ya watu wengine kwani
kufanya hivyo ni kushindana na dola na kutolea mfano wa machafuko
yanayoendelea kwa baadhi ya Nchi Duniani na kupelekea mataifa hayo
kutokalika kutokana na vurungu za kisiasa.
Aidha
amewaomba vijana kutokubali kulitia doa Taifa, kwani Tanzania
inafahamika ni kisiwa cha Amani Duniani na inapaswa kulinda heshima hiyo
ili kuendelea kutunza amani ya Watanzania wote bila kujali tofauti za
kisiasa.
Amewaomba
viongozi hao wa kisiasa kuwasilisha malalamiko yao kwa njia tofauti
kwani Serikali iliyopo madarakani ni sikivu na ipo kwa ajili ya wananchi
wote.

0 comments:
Post a Comment