Frank Mvungi-Maelezo
Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kufanya kazi zao kimkakati ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao hasa kwenye kipindi hiki cha Awamu ya Tano.
Akizungumza leo Jijini Dar es salaam na Wakuu wa Vitengo
vya Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisi za Serikali Waziri wa
zamani wa Habari wa Jamhuri ya watu wa China, Mhe. Zhao Qizheng amesema
ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa mawasiliano yote yanalenga
kuwainua wananchi wake.
“Msemaji wa Serikali inabidi uwe makini katika kazi zako kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati”, alisema Qizheng.
Akifafanua
Mhe. Qizheng amesema kuwa ili Tanzania Iweze kufikia maendeleo ya kweli
ni muhimu kujenga mfumo dhabiti wa Mawasiliano ya Serikali kwa Umma.
Katika
kutekeleza majukumu yao Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini
kama wasemaji ni lazima wawe na uelewa mpana kuhusu masuala yanayohusu
sekta wanazosimamia ili kutoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa wananchi.
Pia
aliwataka Wasemaji wa Serikikali kujiandaa kabla ya kujibu hoja
mbalimbali za kitaifa na Kimataifa zinazohusu Serikali na wananchi ili
kutoa taarifa sahihi kwa Vyombo vya haabari.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Hassan Abbas
amesema ni dhamira ya Serikali kuwasiliana kimkakati ili kuchochea
maendeleo.
“Lengo
letu ni Kuhakikisha kuwa tunafanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa
mawasiliano ya Serikali na wananchi ili kuwapa fursa ya kutoa
mrejesho”alisema Abbas.
Katika
kuhakikisha azma hiyo inatumia Abbas amebainisha kuwa kwa sasa Serikali
inajipanga kufanya maboresho ya mifumo ya Mawasiliano ya Serikali.
Aidha
Mawasiliano ya Serikali katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya
Tano yanalenga kubadilisha maisha ya wananchi kutoka hali duni kwenda
kwenye hali bora.
Mkutano
kati ya Waziri wa Zamani wa Habari wa China na Wakuu wa Vitengo vya
Mawasiliano Serikalini wa Wizara na Taasisis za Serikali umelenga
kujenga uwezo wa Wasemaji wa Serikali ili waweze kuwasiliana na Wananchi
kimkakati.
0 comments:
Post a Comment