Na
Godfriend Mbuya
Kesho
Jumamosi Septemba 24 ni Fainali za Shindano la Dance100% linaloendeshwa na
EATV, ambapo fainali zitafanyika katika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini
Dar es salaam kuanzia saa sita mchana.
Akizungumza
kuhusu maandalizi ya shindano hilo Mratibu Bhoke Egna amesema , mambo yote
yanayohusu shindano yamekamilika ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita
cha shilingi milioni 7.
“Maandalizi
yamekamilika ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na milioni 7 na tunatarajia kuwa
na Jaji mpya atakayeshirikiana na majaji wengine ambapo Msanii wa Bongo Flava
Ali Kiba atashiriki kazi hiyo” Amesema Bhoke.
Kwa
upande wake Jaji wa shindano hilo Super Nyamwela amesema , majaji wameweza
kuwatembelea washiriki wa shindano hilo na kuwaelekeza mambo ya msingi ya
kuzingatia.
“Tumewaelekeza
mambo ya kuzingatia na kwa kweli wamejiandaa vizuri na fainali zitakuwa na
ushindani wa hali ya juu sana hivyo tunawaalika wananchi wote kuja kwa wingi
kutizama vipaji vya wasanii hawa” Amesema Nyamwela.
Shindano
la Dance100% 2016 kesho linafikia tamati kwa mwaka huu ambapo shindano
limedhaminiwa na Vodacom kwa kushirikiana na Coca – Cola , na matukio yote
yataonyeshwa na EATV siku ya Jumapili saa moja jioni.
0 comments:
Post a Comment