Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo amewaahidi Wafanyakazi wa
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufuatilia malimbikizo ya mishahara
yao na kuhakikisha wanalipwa.
Kauli
hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa
Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC )
uliyolenga kujadili bajeti ya mwaka 2016/2017 iliyopitishwa na Bunge na
kuweka mikakati ya namna Shirika litakavyoweza kupata pesa nakuweza kujiendesha pamoja na namna ya kuboresha huduma ya matangazo.
“Natambua
TBC ina wafanyakazi zaidi ya mia sita (600) nawasihi mtakapotoka hapa
mkawarejeshee wenzenu mliyojifunza na mkawaeleze mipango mliyoamua kwa
niaba yao,”alisema Mhe.Anastazia.
Akiendelea
kuzungumza katika Mkutano huo Mhe.Anastazia aliupongeza uongozi wa TBC
kwa kuandaa Harambee ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi
lililotokea Mkoani Kagera kwani wameonyesha uzalendo wao wa kuona
changamoto zilizopo katika kurekebisha miundombinu iliyoharibika pamoja
na kuwasaidia wakazi walioathirika mahitaji muhimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mtendaji Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Ryoba alisema
shirika lina malengo ya kuwafikia Watanzania wote na kuhakikisha
linawaunganisha kwa Taarifa mbalimbali,pamoja na kuandaa vipindi vyenye
maudhui yanayogusa watu wote.
Pamoja naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi RAAWU Taifa Bw.Felician Maige alimuomba Mhe.Naibu Waziri kuzungumza
na uongozi wa Shirika hilo kuhusu kuwapatia ajira za kudumu au mikatabu
baadhi ya wafanyakazi waliyofanya kwa muda mrefu kama vibarua.
Kwa upande wa mmoja wa Wafanyakazi wa TBC Bw.
Asheri Chilewa alimuomba Naibu waziri huyo kupitia Wizara yake na
Taasisi yake ya Kiswahili kuundwe mkakati utakaosaidia kufundisha jamii
lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kwani kwa hivi karibuni kumekuwa na
upotoshwaji wa matumizi ya lugha hiyo kwa kiasi kikubwa na maneno
kutumika isivyo sawa .
Huku akitoa mfano wa namna watu wanasema mtu amepoteza maisha pale anapofariki ambapo siyo sahihi kwani maisha ya mtu hayapotei.
Hata
hivyo Naibu Waziri aliueleza Uongozi wa TBC kuwa Serikali inaelewa
changamoto wanazopitia na kwa sasa inashughulikia suala hilo kwa kuona
ni namna gani kupitia mapato ya Kampuni ya Startimes yatakavyoweza
kuchangia uendeshaji wa shirika hilo na mpaka mwakani mkakati huo
utakuwa umekamilika.
0 comments:
Post a Comment