Na Lilian Lundo-MAELEZO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa
kuzindua ndege mbili za Shirika la Ndege la Tanzania (ATC)
zilizonunuliwa kwa kutumia kodi za wananchi.
Uzinduzi
huo unatarajiwa kufanyika kesho Septemba, 28 mwaka huu katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1).
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu (Uchukuzi), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Dkt. Leonard Chamuriho leo jijini Dar es Salaam alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa ndege hizo.
Dkt.
Chamuriho alisema kuwa ndege ya kwanza iliwasili nchini tarehe
20/09/2016 na ndege ya pili inatarajiwa kuwasili nchini leo tarehe
27/09/2016 kuanzia saa 6:00 mchana.
Vile
vile Katibu Mkuu huyo alisema kuwa ndege hizo zimenunuliwa na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhudumia wananchi wa ndani ya
nchiya Tanzania na nchi jirani.
“Ndege
hizo aina ya Dash 8 Q400 zimetengenezwa na kiwanda cha Bombadier nchini
Canada ambapo kila moja ina uwezo wa kubeba abiria 76 na zitatumika
katika kuhudumia soko la ndaniya Tanzania na nchi jirani,” alifafanua
Dkt. Chamuriho.
Aidha,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawakaribisha wananchi
wote kushuhudia uzinduzi wa ndege hizo unaotarajiwa kuanza saa mbili
kamili (2:00) asubuhi.

0 comments:
Post a Comment