Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dar es Salaam
6.9.2016
SERIKALI
imeanza kupokea maoni na ushauri kutoka kwa asasi za kiraia, sekta
binafsi na wananchi kuhusu maboresho ya rasimu wa mpango kazi wa kitaifa
wa uendeshaji wa shughuli za Serikali kwa uwazi wa Awamu ya tatu
(2016/17 -2017/18).
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Susan Mlawi Ilisema mwisho wa kuwasilisha maoni na ushauri huo ni tarehe 10 Septemba mwaka huu saa 9:30 alasiri.
Mlawi
alisema mpango kazi huo utahusisha vipaumbele katika maeneo saba ambayo
ni pamoja na upataji taarifa, takwimu huria, bajeti za wazi, uwazi
kuhusu ardhi, uwazi kuhusu tasnia ya uziduaji, uwazi katika masuala ya
afya, na mifumo ya utendaji kazi.
Aidha
aliongeza kuwa maoni, ushauri na mapendekezo hayo yanaweza kuwasilisha
Serikalini katika njia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo tovuti rasmi
ya wananchi (www.wananchi.go.tz), tovuti ya ogp (www.opengov.go.tz), government open data portal (www.opendata.go.tz).
Mlawi
alizitaja njia nyingine za kuwasilisha maoni hayo ni katika barua pepe
ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (ps@utumishi.go.tz ) pamoja na njia ya barua kupitia sanduku la posta 2483 Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mlawi alisema rasimu ya mpango kazi inapatikana katika tovuti ya wananchi (www.wananchi.go.tz), tovuti ya ogp (www.opengov.go.tz), government open data portal (www.opendata.go.tz), tovuti ya ofisi ya Rais, menejimenti ya utumishi wa umma (www.utumishi.go.tz), pamoja na mitandao ya kijamii ya facebook (utumishi week) na blog (http://utumishiweek.blogspot.com).
“Moja
ya vigezo na matakwa ya utekelezaji wa mpango huu kwa nchi mwanachama
ni kuandaa mpango kazi wa kitaifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
zikiwemo Asasi za kiraia, sekta binafsi na wananchi, hivyo Serikali
inawahimiza wadau kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao” alisema Mlawi.
Mpango
wa uendeshaji wa Serikali kwa uwazi ni jitihada za kimataifa katika
kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa
wa wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji huduma
bora kwa wananchi. Tanzania ilijiunga na mpango huo mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment