Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Shirika la ndege Precision Air larudisha safari zake za nchini Comoro

Shirika la ndege Precision Air larudisha safari zake za nchini Comoro


Na Godfriend Mbuya
Shirika la ndege la Precision Air, limerudisha rasmi safari zake za kuelekea HAHAYA nchini Comoro kuanzia leo tarehe 27 Septemba 2016.
Ndege kuelekea Comoro iliondoka saa 4 asubuhi kuelkea HAHAYA na ilitarajiwa kuwasili huko saa 5 Asubuhi. Precision Air ilisitisha safari hizo mnamo mwaka 2014 na kutangaza kuzirejesha mapema mwezi  Agosti mwaka huu.
Akizungumzia kurejeshwa kwa safari hizo Mkurugenzi wa biashara wa shirika hilo  Robert Owusu amesema kuwa  Precision Air imejipanga kutoa huduma ya uhakika ya usafiri wa anga kati ya Tanzania na Comoro, ambayo itarahisisha biashara na safari kati ya nchi hizo.
“Safari zetu zitakua kila siku ya Jumanne,  Alhamisi na Jumamosi  ratiba hii imepangwa mahususi kukidhi mahitaji ya safari za kiserekali, kibiashara na hata zile za mapumziko na  kulingana na mapokeo ya soko tunatarajia kuongeza safari zaidi.”  Amesema  Owusu amedokeza.
 “Tunafuraha kurudisha safari hizi kama tulivyo ahidi , na hii itakua sehemu ya 13 katika mtandao wetu kwa ujumla na ni ya pili kwa safari zetu za kikanda.
 Nimatazamio yetu kutengeneza mtandao wa safari ambao utawawezesha abiria wetu kuunganisha safari zao ndani ya Afrika Mashariki, Africa na Duniani kwa ujumla. Tunajivunia kuwa na mtandao bora ziaidi unaowapa wateja urahisi wa kuunganisha safari zao na hatutachoka kuuboresha kuhakikisha tunaendana na matakwa ya soko.” Amesisitiza  Owusu.

 Precision air ndilo shirika pekee la Kitanzania lilo chini ya umoja wa Mashirika ya Ndege Duniani IATA na hivyo huwawezesha abiria kufanya booking zao na kuunganisha na mashirika mengine ya Kimataifa.
Aidha  kwa safari za ndani Precision Air inasafiri kwenda sehemu 13 ikitokea Dar es Salaam kuelekea Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Bukoba, Musoma, Tabora, Kigoma, Mtwara, Zanzibar and Pemba.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa