Na Godfriend Mbuya
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema anampongeza Naibu
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kwa namna ambavyo aliongoza bunge la
bajeti ambalo lilidumu kwa siku 70 wakati ambapo yeye muda mwingi
alikuwa kwenye matibabu nchini India.
Akizungumza kabla ya
kuanza kwa maswali na majibu katika mkutano wan ne wa Bunge la 11 la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Spika Ndugai ametumia fursa hiyo
kuwashukuru wabunge na umma kwa namna walivyomwombea akiwa kwenye
matibabu na hatimaye kurejea salama.
“Ninampongeza Naibu
Spika kwa namna alivyoongoza Bunge akishirikiana na viongozi wengine,
kazi aliyofanya ni ya kupigiwa mfano kwa bunge lililodumu kwa siku 70
kuanzia April 19 hadi Juni 30 mwaka huu” Amesema Ndugai.
Aidha Spika Ndugai
amewata waqbunge wote wa Bungen la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kushirikiana katika kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kibunge.
Katika mkutano wa leo
maswali mbalimbali katika wizara za maji, afya, sheria, kilimo.
Mawasiliano yamweza kuulizwa na wabunge na kupatiwa majibu na serikali.
0 comments:
Post a Comment