Mkurugenzi
Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko akizungumza na wadau mbalimbali walio katika Mapambano dhidi ya Ukimwi leo jijini Dar es salaam. Mkurugenzi huyo amekutana na wadau hao kwa mara ya kwanza kuzungumza nao kuhusu mikakati mbalimbali ya kudhibiti Ukimwi.
Wadau kutoka mashirika
na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko alipokuwa akizungumzanao leo jijini Dar es salaam.
Na. Aron
Msigwa – Dar
es salaam.
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imewataka baadhi
ya wadau, mashirika na taasisi zilizo katika mapambano dhidi Ukimwi kuzingatia
malengo ya awali ya kuanzishwa kwa taasisi hizo
na kuepuka kujiingiza katika shughuli za uanaharakati ambazo ni kinyume
cha sheria.
Akizungumza katika kikao chake cha kwanza na wadau
mbalimbali walio katika mapambano dhidi ya Ukimwi leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi
Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa baadhi ya wadau, mashirika
na taasisi zimekuwa zikifanya shughuli nje ya malengo ya awali ya kuanzishwa hali
inayosababisha mgongano katika jamii.
"Zipo baadhi ya taasisi zinazofanya shughuli nje
ya malengo, tunatambua Serikali haijakataa jitihada za makundi mbalimbali ya
kupambana na UKIMWI, sisi kama TACAIDS tutaendelea kuungana na Serikali kuhakikisha
kuwa zile taasisi zilizo kwenye mapambano zinasimamia malengo ya kuanzishwa
kwake na si vinginevyo" Amesisitiza
Dkt. Maboko.
Amewataka wadau na mashirika hayo kuendelea kujikita na
kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ,uhamasishaji wa wananchi kupima kwa
hiari VVU kwa lengo la kujua hali zao ili
waweze kujikinga na maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Pia amewata wadau hao kuangalia namna bora ya kuwafikia,
kuwaelimisha na kuwafuatilia wananchi walio katika makundi maalum kwenye
mazingira hatarishi pia kuongeza shughuli za utafiti zitakazoisaidia nchi
kufikia lengo la maabukizi sifuri.
Amesema hali
ya uelewa wa wananchi juu ugonjwa wa Ukimwi imefikia asilimia
90 kwa kuwa watanzania sasa wanauelewa kuhusu ugonjwa huo na hali zao . Aidha, wengi
wana uelewa iwapo wamepata maambukizi au la kutokana na kuongezeka kwa kampeni
za uhamasishaji na elimu ya kujikinga na maambukizi.
Kwa upende
wake Mkurugenzi wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania
(UMATI), Lulu Ng’wanakilala amesema Taasisi zinazosajiliwa kutoa huduma za
kuzuia na kupunguza maambukizi dhidi ya Ukimwi nchini Tanzania na kuanza
kujiingiza kwenye shughuli za uanaharakati zinakwamisha na kupunguza juhudi za
Serikali na wadau wengine wenye mapenzi mema walio kwenye mapambano dhidi ya
Ukimwi.
‘Sisi kama wadau wa hizi taasisi tunaongea lugha moja,
NGOs zinazosajiliwa kutoa huduma na kuanza kufanya uanaharakati kupitia masuala
ya Ukimwi zinakwenda kinyume cha maelengo,sisi tupo kwa lengo moja kuhakikisha
maambukizi yanafikia sifuri kwa kuhakikisha wote wanaotakiwa kupata huduma wanafikiwa
na huduma zetu hasa makundi yanayochangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya
Ukimwi’ Amesisitiza.
Naye Afisa
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania
(NACOFA) Bw. Deogratius Peter, akizungumzia hatua ya baadhi ya taasisi kuenenda
kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake amesema
‘Serikali imeshatoa Sera na miongozo mbalimbali inayosimamia
shughuli za utoaji wa huduma za mapambano dhidhi ya Ukimwi kwa taasisi, makundi
na wadau mbalimbali, Sisi pamoja na Serikali
tunakubali na kuheshimu juhudi za makundi haya katika mapambano dhidi ya Ukimwi,
suala la uanaharakati halikubaliki maadili lazima yazingatiwe katika utoaji wa
huduma zetu tufuate sheria za nchi ile kuepusha migongano isiyo ya lazima’
Amesisitiza.
Ameongeza kuwa taasisi zote zilizo katika mapambano
dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi lazima zikajikite katifa tafiti pia kuyafuatilia
makundi yote yaliyo katika mazingira hatarishi ambayo yanachangia kwa kiwango kikubwa kueneza maambukizi ya VVU.
|
0 comments:
Post a Comment