Na Adili Mhina.
Tume
ya Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa pamoja na Sekretarieti ya
Jumuiya ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) imeendesha warsha ya kujenga
uelewa juu ya Dira na mipango ya maendeleo ya kimataifa na kikanda.
Warsha
hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa kituo cha mikutano cha Mwalim
Julius Nyerere, Dar es salaam imewakutanaisha wakurugenzi wa mipango na
sera kutoka sekta mbalimbali, idara na mashirika ya Umma, wawakilishi wa
asasi zisizo za kiraia, wawakilishi wa mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali pamoja na wataalam kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC).
Akifungua
warsha hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Balozi Innocent Shiyo alieleza kuwa Tanzania imekuwa mstari
wa mbele katika kutekeleza makubaliano mbalimbali kikanda na kimataifa
kwa lengo la kutumia fursa zinazopatikana kwa nchi wanachama ili
kuongeza kasi ya maendeleo.
Balozi
Shiyo alieleza kuwa ni muhimu wadau wanaohusika na masuala ya sera na
mipango nchini kuwa na uelewa wa kutosha juu ya namna sera, mikakati na
mipango ya maendeleo ya kimataifa na kikanda iliyofungamanishwa na ile
ya kitaifa ili kuhakikisha utekelezaji wake unaenda sambamba.
“Tanzania
ni mwanachama wa umoja wa mataifa na ipo mstari wa mbele katika
kutekeleza makubaliano mbalimbali ikiwemo agenda ya maendeleo endelevu
2030, programu ya kutekeleza makubaliano ya Instanbuli (2010-2020), nk.
Vile vile ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Nchi
za Kusini mwa Afrika, nk. Hivyo, ni muhimu kujua malengo ya jumuiya hizi
na kuangalia namna mipango yetu ya ndani inavyotusaidia kufikia malengo
ya nje”, alisema.
Naye
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Klasta ya
Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Paul Sangawe alisema kuwa
warsha hiyo itasaidia kujenga uelewa juu ya Sera, mikakati na mipango ya
maendeleo ya kimataifa na kikanda hususani malengo ya maendeleo
endelevu 2030, Agenda ya maendeleo ya Afrika 2063, na mpango mkakati wa
nchi za kusini mwa Afrika 2016/17-2010/21.
Aliongeza
kuwa warsha hiyo itasaidia kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya
utekelezaji wa sera, mikakati na mipango ya maendeleo ya kimataifa na
kikanda.
0 comments:
Post a Comment