Kampuni
ya Vodacom imezitaka klabu za Simba na Yanga kuwaburudisha watanzania katika
mchezo wa Jumamosi hii katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam
Akizungumza
na EATV Jijini Dar es salaam kwa niaba ya Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini
wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, Mkuu wa Kitengocha Masoko cha Masoko na
Mawasilino, Nandi Mwiyombella amesema wakiwa kama Vodacom wanazitakia kila la
kheri timu za Simba na Yanga katika mchezo wa Jumamosi Octoba Mosi 2016.
“Simba
na Yanga zinapambana katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara
Jumamosi hii, sisi kama Vodacom na wadhamini wakuu wa ligi hii tunawatakia kila
la heri na tunaamini kwamba mchezo wao utakuwa ni burudani tosha kwa mashabiki
wa soka hapa nchini” Amesema Nandi.
Nandi
ameongeza kuwa Vodacom inaamini kwamba mchezo huo utakuwa mzuri na
wakuburudisha na inawaondoa hofu mashabiki wote ambao watafika uwanjani kwani
ni mara ya kwanza kwa msimu huu kwamba watafurahia viwango vitakavyooyeshwa na
pande zote mbili.
Aidha
mashabiki ambao hawatafanikiwa kufika uwanjani wanaweza kupata matokeo hayo
‘live’ kwa kujiunga na kifurushi cha ‘soka bando’ kifurushi ambacho
kinapatikana kwa shilingi 500 na kinatoa fursa kwa wanamichezo kupata matokeo
ya mechi kati ya Simba na Yanga na ni kifurushi kwa ajili ya mashabiki wa soka
ambapo unaweza kupata matokeo ya mechi popote pale ulipo na dakika 14 za kupiga
Vodacom Kwenda Vodacom na dakika 2 kwenda mitandao mingine pia utapata sms 20
kwa masaa 24.
,Pia
napenda kuwatoa wasiwasi wapenzi wa mchezo huu ambao hawatapata na nafasi ya
kufika uwanjani kwani Vodacom Tanzania haitawaacha mbali na
Ili kununua kifurushi
hiki anachotakiwa kufanya mteja ni kupiga namba *149 * 01#, Ofa mpya
alafu chagua ‘Soka Bando’. Baada ya hapo mteja atapata ujumbe
unaomtaka ajisajili kwa timu ya soka anayoishabikia kwa kutuma jina la timu
mfano “Yanga” “Simba” au “Azam” nk. kwenda namba 15460
0 comments:
Post a Comment