Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia
wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam.
Katika matembezi hayo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kimepatikana.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj
Ally Hassan Mwinyi akizungumz wakati wa kufungua rasmi Matembezi ya Hisani kwa
ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo
Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja
vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi
1,502,680,000/= zilichangwa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine
Mahiga akizungumza na washiriki wa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia
wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam.
Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa
wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/= zilichangwa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza Matembezi
ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For
Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga, Mwenyekiti wa
Wabunge kutoka Kagera, Profesa Anna Tibaijuka na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akizungumza katika hafla ya kuchangia
wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera
iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu leo Jijini Dar es
Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha
shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.

Naibu Waziri wa Nchi, OWM –Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Mhe. Abdallah Posi akizungumza katika hafla ya kuchangia wahanga wa
Tetemeko lililotokea mkoani Kagera
iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu leo Jijini Dar es
Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Matembezi ya Hisania ambapo kiasi cha
shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.
Baadhi ya washiriki wa hafla ya kuchangia
wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera
iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu wakifuatilia mtukio
katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilitanguliwa na
Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= zilipatikana.

Wawakilishi wa Jumuiya ya Wabohora
nchini wakimkabidhi Rais Mstaafu wa
Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan
Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya
kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera kwa Rasi wakati wa Matembezi ya
hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF Bw. William Erio na Afisa
Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa
hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia wahanga wa
Tetemeko Mkoani Kagera wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini
Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Waziri wa Mmbo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Alhaj Ally Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashari katika kufanikisha Matembezi ya
hisani ya “ Walk for Kagera” Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Busemaker
akipokea cheti kwa ajili ya kutambua udhamini wa Benki hiyo katika kufanyikisha
matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Kagera leo
Jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Alhaj Ally Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki katika kufanikisha Matembezi ya
hisani ya “Walk for Kagera” Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Aziz Mlima leo
Jijini Dar es Salaam.
ais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiagana na baadhi ya washiriki wa Matembezi ya Hisani
kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo
Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja
vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi
1,502,680,000/= zimechangwa.Picha
na Frank Shija, MAELEZO.
Na: Frank Shija, MAELEZO
TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5 zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu mjini Bukoba Mkoani Kagera.
Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani.
“Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati.
Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikali pamoja na Taasisi zake imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.
“Najua kuna athari kubwa imetokea kutokana na tetemeko hili, sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapata misaada na kurejesha huduma zote katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.
Awali akisoma maelezo ya tathmini ya athari za tetemeko hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi ya vifo ni 17, nyumba zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo 44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania pale panapo hitaji msaada wao.
Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.
0 comments:
Post a Comment