Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MSEMAJI WA SERIKALI: TUTAENDELEZA UHUSIANO NA USHIRIKIANO NA VYOMBO VYA HABARI

MSEMAJI WA SERIKALI: TUTAENDELEZA UHUSIANO NA USHIRIKIANO NA VYOMBO VYA HABARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 




Na Beatrice Lyimo
MAELEZO
Dar es Salaam
27.10.2016.

SERIKALI imeahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano na vyombo vya habari nchini ili kuviwezesha kutelekeleza vyema wajibu wake kwa umma.

Akizungumza katika wakati tofauti wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi za Vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari Hassan Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa chachu ya maendeleo ya wananchi nchini.

Aliongeza kuwa yapo mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Serikali katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo umeme, maji, barabara, afya, elimu, ambapo taarifa za utekelezaji wa ahadi hizo za Serikali hazijaweza kuandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari.

Abbas alisema katika kuimarisha mfumo wa utoaji wa habari na taarifa kwa umma, ofisi yake kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) wameanzisha kipindi cha TUNATEKELEZA ambacho kinatoa fursa kwa Viongozi wa Serikali kutoa taarifa kwa umma kuhusu utelekezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali.

Aidha Abbasalisema ofisi yake ndiye msimamizi na mratibu mkuu wa vitengo vya mawasiliano Serikali, hivyo alitoa wito kwa wanahabari kuwasiliana naye mara kwa mara pindi wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa taarifa katika ofisi za umma.

Kuhusu mafunzo kwa wanahabari, Abbas alivitaka vyombo vya habari kutumia fursa ya waandishi wakongwe waliopo katika ofisi zao, ambao wamebobea katika maeneo mbalimbaloi ikiwemo uandishi wa makala, habari na upigaji picha.

Kwa mujibu wa Abbas alisema kwa sasa, ofisi yake inaendelea na zoezi la kuwahamasisha Maafisa Habari wa Serikali katika Wizara, Idara, Taasisi, Wakala, Mikoa, na Wilaya nchini kuanza mageuzi katika mfumo wa taarifa kwa umma ikiwemo kutumia mitandao ya kijamii.

MWISHO 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa