NA EVELYN MKOKOI  - DSM
Tawi la baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya
makamu wa Rais limetakiwa kuwa ndo sehemu sahihi ya kujadili na kutatua migogoro
ya wafanyaki na siyo majukwaa ya siasa.
Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi
anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe January Mkamba, Lipokuwa
akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais
Mtaa wa Luthuli jijini dar  es Salaam.
 Mhe.Makamba
alisema kuwa vikao vya baraza la wafanyakazi vimekuwepo kisheria na ni muhimu
wajumbe kukaa pamoja kujadili masuala ya msingi yanyowahusu watumishi kwani wao
ndo waliowachangua hivyo, majadiliano yanayokuwepo  katika vikao hivyo ni nyenzo muhimu ya kuondoa
migogoro na migomo mahala pa kazi.
. 
“Nyie ni miongoni mwa watumishi wa Ofisi ya
Makamu wa Rais ambao kwa namna moja au nyingine mmeaminiwa na kukabidhiwa
dhamana ya kuwawakilisha wenzenu katika chombo hiki muhimu, katika kuamua na
kushauri Baraza juu ya masuala mbalimbali yanayolenga kuleta ufanisi na utulivu
ndani ya Ofisi yetu.alisisita Makamba”.
Aidha, Waziri Makamba alisema kwamba, Lengo
la vikao vya Baraza ni kuleta ufanisi wa utendaji kazi mahala pa kazi kwa ajili
ya manufaa ya Taifa  kuelekezana,
kushauriana na kukumbushana, kuhusu majukumu ya ofisi  na ushiriki wa wafanyakazi katika kuyatekeleza
na kuyasimamia, na aliongeza kwa kusema kuwa  ni fursa ya kipekee ya kutafakari utendaji wa
kazi na majukumu ya Ofisi kwa ujumla.
Kikao
hicho cha baraza la wafanyakazi cha Ofisi ya makamu wa Rais kimudhuriwa na wawakilishi
kutoka TUGHE Taifa na Mkoa na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
Zanzibar. 

0 comments:
Post a Comment