Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SERIKALI YAHAIDI KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA KWA UONGOZI MPYA WA TUCTA

SERIKALI YAHAIDI KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA KWA UONGOZI MPYA WA TUCTA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


SERIKALI YAHAIDI KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA KWA UONGOZI MPYA WA TUCTA.
Na Daudi Manongi-MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, Jenister Mhagama amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) ili kuleta tija na ufanisi katika sekta ya kazi.
Waziri Mhagama aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Viongozi hao wa TUCTA waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa shirikisho hilo.
“Tumefarijika sana kwa TUCTA kupata uongozi mpya ambao tuna uhakika wanachama wamezingatia masuala  muhimu katika uchaguzi wao ikiwemo weledi na kutazama dira ya sekta ya wafanyakazi nchini”.
Aidha aliongeza kuwa Viongozi hao wana jukumu kubwa la kuleta tija na maendeleo chanya katika sekta ya kazi nchini na kuhimiza kuwa wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi.
Kwa mujibu wa Mhagama ameahidi Viongozi hao kufanya kikao kazi mapema iwezekanavyo kwani uchaguzi umekwisha na sasa kilichobaki ni kufanya kazi.
Pia amesisitiza ushirikiano wa kudumu kati ya Serikali, Waajiri na wafanyakazi ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro iliyopo.
Kwa upande wake Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamghokya alimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kusimamia utu wa mtumishi kwa kuhaidi kuwalinda kutokana na baadhi ya viongozi kutoa lugha zisizosahihi.
Aidha, ameishukuru Serikali kwa kuwa karibu nao kwa muda wote na kuhaidi kuendeleza ushirikiano huo ili kuleta tija katika kazi.
MWISHO



0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa