Home » » SERIKALI YAKANUSHA UWEPO WA UGONJWA WA ZIKA NCHINI

SERIKALI YAKANUSHA UWEPO WA UGONJWA WA ZIKA NCHINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na Ally Daud-MAELEZO
Serikali imeendelea kukanusha taarifa za uwepo wa ugonjwa wa zika nchini kuafuatia uwepo wa taarifa za ugonjwa huo zilizosambaa mwishoni wa wiki hii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kufanya mazoezi uliofanyika leo jijini Dar es salaam Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi amesema kuwa hakuna ugonjwa wa zika wala mtu aliyethibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo.
“Ule ulikua utafiti  wa awali wa kujaribu kipimo cha kupima ugonjwa wa zika na si vinginevyo kama taarifa zilivyoenea hivi karibuni nchini”alisema Prof. Kambi.
Aidha Dkt. Kambi amesema kuwa Watanzania waondoe wasiwasi ila wajikinge zaidi ili kuepuka kabisa ugonjwa huo usiingie nchini kwa ajili kujenga taifa lenye wananchi wenye afya imara.
Mwisho.


 

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa