Meneja
mradi wa ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Mhandisi Mwanaidi Mkwizu (aliyevaa suti) akitoa melezo kwa Timu
ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango.
Na Adili Mhina, DSM.
Tume ya mipango imefanya ziara katika mradi wa ujenzi wa jengo la III la abiria katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (Terminal III) jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi huo na kuelezwa kuwa ujenzi umefikia asilimia 65.
Akitoa
maelezo mbele ya timu ya wataalamu kutoka Tume ya Mipango, Meneja wa
Mradi huo Mhandisi Mwanaidi Mkwizu alieleza kuwa ujenzi huo unaotekelezwa
na Mkandarasi wa kampuni ya BAM kutoka Uholanzi ulioanza Juni 2013 na
unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba Mwaka 2017.
Akielezea
miundombinu ya uwanja huo, Mhandisi Mkwizu alisema kuwa uwanja huo wa
kisasa una barabara ya kuruka ndege (runway) yenye urefu wa kilometa 3
na upana wa mita 60 ambapo upana unaohitajika kwa matumizi ya ndege ni
mita 45.
Aliongeza
kuwa mradi huo pia umeangalia changamoto ya kukatika umeme mara kwa
mara na kuamua kutafua vyanzo mbalimbali ili kuondokana na utegemezi wa
chanzo kimoja ambacho kinaweza kukwamisha shughuli katika uwanja huo
pale inapotokea hitilafu.
Alieleza kuwa kutakuwa
na njia mbili tofauti za kuleta umeme kutoka TANESCO ambapo njia moja
ni kwa ajili ya dharura na pia endapo kutakuwa na tatizo la kukatika
umeme kupitia njia za TANESCO, umeme utapatikana kutoka chanzo mbadala
cha dharura kwa kutumia jenerata nne kubwa za kisasa za dizeli zilizopo
eneo la mradi ambazo zinatosha kukidhi mahitaji ya eneo hilo.
Alisisitiza kuwa tayari wamefanya mazungumzo na TANESCO na kukubaliana kuwa njia hizo za umeme ni kwa ajili ya uwanja huo pekee na hakuna wateja wengine watakaounganishiwa katika njia hizo.
Mhandisi
mkwizu alimalizia kwa kusema kuwa yeye pamoja na timu yake ya wataalamu
wanaendelea kufanya usimamizi wa karibu ili kuhakikisha kuwa
utekelezaji wa mradi huo unaenda sambamba na malengo yaliyopangwa.
Wataalamu
wa ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango walipata fursa ya
kutembelea maeneo mbalimbali ya ujenzi wa mradi huo na kuonesha
kuridhishwa na kasi yautekelezaji huku wakimshauri menejea wa mradi huo
kuendelea na ufanisi wake katika kusimamia kazi hiyo ili kuhakikisha
malengo ya mradi huo yanafikiwa.
0 comments:
Post a Comment