NA EVELYN MKOKOI -DSM
Akiwa katika siku nyingine ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar
es salaam, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina, leo ametembelea katika Maeneo ya keko Magurumbasi na kujionea
namna ambavyo wamiliki wa viwanda wanavyotiririsha maji katika mfereji maarufu
kwa jina la mseleleko.
Baada ya ukaguzi wa mazingira katika maeneo hayo, Naibu
Waziri Mpina amewaasa wawekezaji wenye viwanda nchini waliojenga juu ya
miundombinu ya majitaka kutafuta njia nyingine ya ujenzi sahihi ya miundombinu
ya majitaka kutoka viwandani mwao kwenda kwenye mfumo wa mamlaka za maji na
kuelekeza kuwa iwapo wataonekana kuziba kwa ujenzi wa majengo yao mitaro
mikubwa ya miundombinu ya maji, sheria itachukua mkondo wake ikiwa ni pamoja na
kubomoa majengo yao.
Akijibu swali la mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha
television hapa nchini, lilihoji kuusika
kwa watumishi wa umma kwa namana moja au nyigine kiujanja ujanja katika
kuruhusu vibali vya ujenzi na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya majitaka na
mazingira kwa ujumla, Mpina alisema kuwa endapo kutagundulika kuwa na ushiriki
wowote wa watumishi wa umma katika suala hilo sheria pia itachukua mkono wake.
Pamoja na hilo Naibu Waziri Mpina amewaeleza wenye viwanda
wanaoendelea kuchafua mazingira kuwa kutakuwa na oparesheni kubwa nchini ya
ukaguzi wa mazingira itakayohusisha halmashauri za miji, mamlaka za maji,
wamiliki wa mabomba ya maji taka na wananchi ili kuwajibika kwa pamoja katika
kunusuru uharibifu wa mazingira.
Aidha Ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
NEMC kuiandikia hati ya zuwio TANROADS ya mwezi mmoja itayowataka wafumue
karavati lao linalopita chini ya barabara katika eneo la kurasini BP darajani
na kuliongeza ukubwa ili majitaka yaweze kupita kwa nafasi.
Naibu waziri Mpina Pia amewataka Viongozi wa Manispaa ya
Ilala kusimamia kikamilifu usafi wa Mazingira na kuwataka wananchi wa eneo la
keko magurumbasi wanaokaa karibu na mfereji wa mseleleko kufanya usafi katika
mfereji huo na kutooutumia kama DAMPO.
Kwa upande wake mratibu wa Mazingirawa kanda ya mashariki
kutoka NEMC Bw. Jaffari Chimgege amesema wao kama Baraza watakaa kwa Pamoja na
wawekezaji, wenye makaravati madogo yanazoshindwa kupitisha majitaka vizuri
jijini DSM na kutafuta suluhisho la kudumu kwani hali hiyo ni hatari hasa
katika kipindi cha mvua, inaweza kusababisha magojwa ya milipuko kama vile
kipindupindu.
0 comments:
Post a Comment