Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
(kushoto), akisalimiana na Mshauri wa Kitengo cha Utafiti wa Udongo kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (BICO,UDSM), Dk. Dalmas Nyaoro, baada ya kuwasili eneo
la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Magereza ambao unakadiriwa kuhifadhi
watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira, akisaini dafrari la wageni baada ya kuwasili kwenye Mradi wa
Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Magereza unaoendelea katika eneo
la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Mradi huo unakadiriwa kuhifadhi
watumishi zaidi ya 300 ukikamilika.
Mratibu
wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza
kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Julius Chego (kulia), akimpa
maelekezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira alipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo katika
eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Mradi huo unakadiriwa kuhifadhi
watumishi zaidi ya 300 ukikamilika.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (katikati), akimpa maelekezo Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa
Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, Julius Chego (kulia)
wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo ambao unakadiriwa
kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga,
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, Dk. Juma Malewa.
Kaimu
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa, akifafanua
jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira (katikati), wakati Katibu Mkuu alipotembelea kukagua
maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi
la Magereza, ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300
ukikamilika katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mratibu Mkuu wa mradi huo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),
Julius Chego.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (aliyevaa Kaunda suti), akiteta jambo na Kaimu Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa wakati alipotembelea
kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa
Jeshi la Magereza, ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300
ukikamilika katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment