Na Jacquiline Mrisho.
Idara
ya Habari (MAELEZO) imebaini nyaraka za kughushi zilizowasilishwa na
Mmiliki wa Kampuni ya FUKANI, Joseph Sheka wakati alipoziwasilisha kwa
ajili ya kusajili gazeti la LETE MAMBO.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa MAELEZO,
Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliwasilisha nyaraka
mbalimbali akidai kuwa ni za Mamlaka ya Mapato (TRA) ambazo uchunguzi wa
awali umebaini kuwa mihuri na sahihi za baadhi ya maafisa wa Mamlaka
hiyo zilizotumiwa ni za kughushi.
“Ni
vyema jamii ikafahamu kuwa huu sio wakati wa kujaribu kuishi kwa njia
zisizo halali, kila mwananchi anapaswa kufuata taratibu zinatohitajika
pindi anapotaka kupatiwa huduma katika maeneo mbalimbali ya ofisi za
Umma.
Dkt.
Abbasi alitoa rai kwa ofisi mbalimbali za Umma kuwa makini na nyaraka
zinazowasilishwa na wateja wao kwani zinaweza kuwa na malengo mbalimbali
ya kuiingiza Serikali katika matatizo hivyo kuitia hasara.
Mbali
na hayo Dkt abbasi alisisitiza kuwa wale wanaohisi waliwasilisha
nyaraka zao na kuona kwamba zina utata kuja kuzirekebisha na
watakaobainika kuwa walighushi nyaraka hizo sheria itafuata mkondo wake.
Kwa sasa Idara ya Habari imemkabidhi mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini dar es salaam kwa mahojiano zaidi.
0 comments:
Post a Comment