Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WAZIRI MAKAMBA ATOA MAELEKEZO KATIKA KIKAO KAZI

WAZIRI MAKAMBA ATOA MAELEKEZO KATIKA KIKAO KAZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akiwasili katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi yake. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi yake.
Sehemu ya Menejimenti timu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba kabla ya kuanza kikao kazi katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) na Eng. Bonaventure Baya Mkurugenzi Mkuu (NEMC) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi katika kikao kazi kinachoendelea katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Bw. Ntime Mwalyambi akiwasilisha mada katika kikao kazi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa