Katibu Mkuu Ofisiya
Makamu wa Rais, Profesa Faustin Kamuzora amemteua Bwana Richard Muyungi
kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi hiyo.
Awali Bwana Muyungi
alikua ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya
Makamu wa Rais. Bwana Muyungi pia ni mjumbe wa Bodi ya Dunia ya mfuko wa
mabadiliko ya tabia Nchi akiwakilisha Afrika. Pia ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Ushauri wa Marais wa Afrika kuhusu masuala ya mabadiliko ya
tabianchi (CAHOSCC)
Uteuzi wa Bwana Muyungi umeanza mara moja tarehe 8/2/2017
0 comments:
Post a Comment