Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Ni
jambo lisilopingika kuwa matumizi makubwa ya fedha za Serikali
yanatumika katika ujenzi wa miundombinu ya Umma ambapo matumizi hayo
yanahusisha karibu asilimia 53 ya Bajeti nzima ya nchi.
Tunaishukuru
Serikali kwa kuweka kipaumbele katika suala hilo kwani ni muhimu kuwa
na miundombinu mizuri na bora ili kutoa huduma bora kwa wananchi na
kurahisisha ufanyaji kazi hivyo kuharakisha maendeleo ya nchi katika
Nyanja zote muhimu zikiwemo za biashara, utalii na mawasiliano.
Miradi
ya ujenzi ya miundombinu ya Umma inayoelezewa hapa ni ile ambayo
inajengwa kwa fedha za Serikali kwa ajili ya matumizi ya wananchi wote
ikiwemo ya barabara, hospitali na vituo vya afya,shule,vyuo,nyumba za
kuishi pamoja na ofisi mbalimbali.
Jitihada
hizo za Serikali kuhakikisha miundombinu ya Umma inaleta maendeleo
imekuwa ikikwamishwa na changamoto mbalimbali zinazojitokeza pindi mradi
husika unavyoanza kwani wahusika wanakuwa wanajiamulia jinsi ya kufanya
ili mradi ujenzi husika umalizike.
Hali
hiyo inapelekea Serikali kupata hasara kwa kupoteza fedha nyingi na
kuambulia kubaki na majengo yasiyo na viwango ambayo mwisho wake
hushindwa kutumika na kuilazimu Serikali kuanza upya ujenzi husika baada
ya kubomoa.
Kwa
kuwa Serikali hii ni sikivu na imejipanga kuhakikisha nchi inafika
katika uchumi wa kati basi tunaamini mambo hayo hayana nafasi na
hayawezi kutokea tena katika nchi hii watu kuachiwa uhuru wa kutumia
vibaya fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.
Tunaamini
kuwa maendeleo ya nchi yanachangiwa na wananchi wenyewe kwa njia ya
ukusanyaji wa kodi na ushuru mbalimbali hivyo hata miundombinu ya umma
inajengwa kwa kutumia fedha za wananchi zinazopatikana kwa njia ya
ukusanyaji mapato.
Hivyo,
ili kuifanya Serikali kuwa na taswira nzuri kwa wananchi wao pamoja na
kuwafanya wananchi kuiamini Serikali yao ni vizuri kuwapa taarifa juu ya
matumizi ya fedha hizo wanazozikusanya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,(Ujenzi), Mhandisi.
Joseph Nyamuhanga amewahi kusema kuwa Sekta ya Ujenzi ni sekta moja wapo
inayoonekana imekithiri kwa rushwa duniani kwa sababu takribani
asilimia 10 hadi 30 ya Bajeti yake inapotea kwa njia ya rushwa na
usimamizi mbaya hivyo ili kuondoa dhima hii ni lazima kukusanya na kutoa
taarifa kwa wananchi juu ya ujenzi wa miundombinu hiyo.
Kuwapa
taarifa wananchi juu ya miradi mbalimbali haswa ya ujenzi wa
miundombinu kutaamsha ile hali ya watu kuona umuhimu wa kulipa kodi kwa
sababu wanaona matumizi ya fedha wanazozikusanya.
Taarifa
hizo pia zitaendeleza uwajibikaji na uwazi katika ujenzi wa miundombinu
hiyo hivyo kupunguza vitendo vya rushwa,kujenga miundombinu inayoendana
na thamani ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi husika pamoja na
kujenga miundo mbinu bora na imara.
Ni
muhimu kwa Serikali kupitia miradi yote iliyojengwa na inayoendelea
kujengwa kwa kutumia fedha za Umma ili kugundua thamani halisi ya
majengo hayo na kutoa taarifa kwa wananchi.
Jambo
hili pia litasaidia vyombo husika vya kisheria kuwachukulia hatua watu
wote walioshiriki kutumia vibaya fedha za wananchi kwa kujenga
miundombinu iliyo chini ya kiwango au isiyoendana na thamani ya fedha
iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi husika.
Rai
inatolewa kwa wizara na idara zinazohusika na ujenzi wa mioundombinu ya
umma kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya mradi upi uko wapi na
unathamani gani ili wananchi waweze kupima kama kiasi walichoambiwa
kimetumika kina thamani ya fedha waliyoambiwa?
Pia
ni muhimu wananchi wakaelimishwa juu ya umuhimu wa kuwa walinzi katika
miundombinu hiyo ili isitokee watu wachache wakuihujumu kwani fedha
nyingi za walipa kodi zimetumika.
0 comments:
Post a Comment