Dar es Salaam, Februari 20, 2017- Kwa mara ya kwanza,
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeanza kuuza nje ya nchi bidhaa
zake katika soko la kikanda, eneo la
kwanza likiwa ni nchi jirani ya Tanzania kwa upande wa Kaskazini,
Kenya.
Shehena ya kwanza ya bia inayofahamika kama Allsopps
ilisafirishwa kwenda Kenya wiki iliyopita na hivyo kukiweka kiwanda cha SBL
kuwa mmoja wachangiaji wakubwa katika soko la kanda.
Akizungumzia kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
SBL, John Wanyancha alisema; “Hii ni hatua nyingine ya
kufurahisha katika kampuni yetu na kimsingi
kwa bidhaa zetu. Ukweli unabakia kwamba kumudu kupenyeza
ndani ya soko la Kenya kunaonesha kuwa ubora wa bidhaa
zetu sio tu kwamba unakubalika na wateja wetu wa ndani
bali pia zinakubalika katika soko kubwa la
kikanda.”
Wanyancha alisema kuwa SBL inaangalia uwezekano wa
kupanua mauzo ya biashara katika masoko mengine ya kikanda, hatua ambayo
iko katika mkondo wa kuhamasisha Jumuia ya Afrika
Mashariki na kada nyingine za kiuchumi kuongeza biashara
yake ya kuvuka mpaka ndani ya ukanda huo.
SBL imekuwa inazalisha aina za bidhaa zinazotambulika
kimataifa kama vile Pilsner Lager,Tusker Lager, TuskerLite, Kibo
Gold, Guinness Stout, Uhuru, The Kick pamoja na bidhaa kuu ya Serengeti Premium
Lager-ambayo peke yake imeshajizolea medali kumi
zinazotambuliwa kimataifa.
0 comments:
Post a Comment