Na Mwandishi Wetu
Wanaharakati
wanaopinga Sheria ya Huduma za Habari iliyopitishwa hivi karibuni
wamepata pigo baada ya mmoja ya wakili Bw. Francis Stolla kujitoa katika
utetezi.
Akiongea
leo Jijini Dar es Salaam Wakili nguli wa Kujitegemea Bw. Stolla alisema
kuwa ameamua kujitoa katika kesi hiyo iliyofunguliwa na wanaharakati
dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutokana na kukabiliwa na majukumu
mengine.
“Wakati
Shauri linafunguliwa Arusha sikuwepo kwa sababu ya majukumu mengine,
pia lilivyofunguliwa Mwanza sikuwepo hivyo kutokana na hilo nimeamua
kuwaachia mawakili wengine waendelee na shauri hilo na mimi niendelee na
majukumu mengine” alisisitiza Wakili Stolla.
Alisema
kuwa madai makubwa ya mawakili hao ni kwamba Sheria ya Huduma za habari
inakiuka mkataba wa Afrika Mashariki, na kusema kuwa kesi
iliyofunguliwa Mwanza inaitaka Mahakama itamke kwamba kuna baadhi ya
vifungu vilivyotajwa kwenye Sheria ya Huduma Habari inakiuka Katiba ya
nchi.
Akiongea
kuhusu dalili za kushindwa kwa kesi hiyo iliyofunguliwa na wanaharakati
dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika mahakama ya haki ya Afrika
Mashariki na Mahakama kuu Mwanza Bw. Francis Stolla alisema suala hilo
anaiachia mahakama kwani ni kinyume kutoa mapendekezo wa kesi kushindwa
au kushinda.
“Mara
nyingi huwa tunaiachia Mahakama na mashauri hayo yote mawili yapo
Mahakamani huwezi sema shauri hili litashinda ama kushindwa kwa sababu
mashauri yakiwa mahakamani haturuhusiwi kusema shauri hili litashinda
ama kushindwa ili Mahakama ibakie kuwa huru” alisema Wakili Stolla.
Kesi
hiyo ilifunguliwa na wanaharakati katika mahakama ya haki ya Afrika
Mashariki mkoani Arusha na Mahakama kuu ya Tanzania Mkoani Mwanza.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment